Habari za Punde

Dkt.Mpango Kufunga Mashindano ya SHIMUTA Mkoani Tanga Novemba.21,2022

 

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya CCM Mkwakwani Jijini Tanga ambacho pia kitatumika katika mashindano ya Shimuta
Mwenyekiti wa SHIMUTA Taifa Roselyne Massam akizungumza kuhusu maandalizi ya mashindano hayo yanayoanza leo Jijini Tanga
Mratibu Mkuu wa Shirikisho hilo Maswet Masinde alieleza namna walivyojipanga kuhakikisha hakuna mamluki atakayechezeshwa kwenye timu zitakazoshiriki mashindano hayo kwani wamejipanga kusimamia sheria kanuni na taratibu zinazowaongoza katika michezo yote.

Na Oscar Assenga,TANGA.
MAKAMU wa Rais Dkt Philip Mpango anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Mashindano ya Mashirika ya Umma,Makampuni na Taasisi Binafasi nchini (Shimuta) Novemba 21 mwaka huu kwenye viwanja vya Mkwakwani Jijini Tanga.
Hayo yalibainishwa leo na Mwenyekiti wa SHIMUTA Taifa Roselyne Massam wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Tanga kuhusu mashndano hayo ambapo alisema kwa mara ya kwanza tokea yalipoanza mwaka huu 2022 yameweka rekodi mpya.

Alisema rekodi hiyo inatokana na kuongezeka kwa idadi ya timu na sasa kufikia 52 zitakazochukua kuwasaka mabingwa kupitia michezo watakayoshindaniwa ambayo itatimua vumbi leo Novemba 15 katika viwanja mbalimbali Jijini hapa

Mwenyekiti huyo alisema amesema tangu wameshika hatamu ya kuliongoza shirikisho hilo haijawahi kutokea kushirikisha timu nyingi zaidi kama mwaka huu jambo ambalo linaonyesha mwitikio umekuwa ni mkubwa na michezo hiyo kuonekana kuleta tija kwa washiriki mashirika, makampuni na taasisi zenyewe wanazotoka.

Naye kwa upande wake Mratibu Mkuu wa Shirikisho hilo Maswet Masinde alieleza namna walivyojipanga kuhakikisha hakuna mamluki atakayechezeshwa kwenye timu zitakazoshiriki mashindano hayo kwani wamejipanga kusimamia sheria kanuni na taratibu zinazowaongoza katika michezo yote.

Mashinde alisema kwamba msimu huu wamekuwa wakali zaidi kuhakikisha wanadhibiti mamluko hivyo wamekwisha kufanya uhakiki kuondoa mamluki kwa kutumia taasisi za umma ikiwemo NHIF, WCF, PSSF kuhakiki washiriki lengo likiwa ni michezo hii iwe ni kwaajili ya watumishi wale ambao wanatambulika kisheria na ili uwe mshiriki unapewa leseni maalumu na lazima uwe umehakikiwa kwenye mifuko hiyo.

Mratibu huyo alisema kwamba mpaka sasa wanamichezo 2183 ambao tayari wameshafika hapa jiji la Tanga na ni namba kubwa ya wanamichezo wanaoshiriki lakini tuna kanuni ambazo zinaongoza katika mashindan pia watatumia kanuni za michezo husika pale inapobidi huku akisisitiza umuhimu wa waamuzi wasimamie sheria taratibu na miongozo inayoongoza michezo husika ili kusiwepo na manung'uniko ya hapa na pale

Akieleza namna mkoa huo ulivyojipanga kuelekea Mashindano hayo Mkuu wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba amesema kwamba mkoa upo salama na kuwahakikishia ulinzi na usalama muda wowote watakapokuwepo kwenye mashindano hayo.

Mkuu huyo wa Mkoa alitumia nafasi hiyo pia kuwataka wakazi wa Tanga wakiwemo wafanyabiashara na wajasiriamali wadogo wadogo kuchangamkia fursa za uwepo wa mashindano hayo kujiongezea kipato.

"Mashindano haya ni zaidi ya michezo yana faida ya kipato lakini yanainua uchumi wa mtu mmoja mmoja na kuongeza pato la taifa, nitoe wito kwa wafanyabiashara wote wachangamikie fursa na kujitokeza kwa wingi katika michezo hii " alisema Mgumba.

"Suala la hali ya ulinzi na usalama liko vizuri tumeendelea kuimarisha doria kwa sababu tumepata ujio wa watu wengi hivyo hali ya usalama iko vizuri tumeendelea kujiimarisha zaidi doria za mchana na usiku kuwahakikishia wanamichezo na wageni wetu wote wanakuwa salama wakati na hata baada ya kumaliza michezo" aliongeza

Michezo itakayochezwa wakati wa mashindano hayo ni michezo ya mpira wa miguu kwa wanaume, mpira wa Pete , Wavu, Kikapu, Dats, Pool table, Vishale , Draft kukimbia kwa magunia, Riadha kuvuta kamba Bao na mingineyo kedekede, lengo kuu hasa ikiwa ni kuimarisha mahusiano baina ya taasisi, mashirika na makampuni kuimarisha afya kupitia michezo ikiwa pia ni kuondokana na magonjwa yasiyoambukiza.

Michezo hiyo ambayo hufanyika kila mwaka ni kwa mara ya pili mfululizo kufanyika ndani ya mkoa wa Tanga mwaka huu yakija na kauli mbiu ya 'SHIMUTA familia moja'.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.