Habari za Punde

IGP Wambura Aagiza Kusimamia Sheria

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini (Mb) akitoa neno mbele ya wajumbe (hawapo pichani) wa kikao cha 16 cha Baraza la Wafanyakazi  wa Idara ya Jeshi la Polisi kilichofanyika leo tarehe 02 Disemba 2022 jijini Dodoma, ambapo aliwataka wafanyakazi kujipanga kimkakati na kutumia fursa ya vikao hivyo kujadili utekelezaji wa bajeti kwa maendeleo endelevu ya Idara ya Jeshi la Polisi. 

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini (Mb) katikati, akimsikiliza Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Camillus Wambura (kulia) baada ya ufunguzi wa kikao cha 16 cha Baraza la Wafanyakazi  wa Idara ya Jeshi la Polisi kilichofanyika leo tarehe 02 Disemba 2022 jijini Dodoma, kushoto ni kamishna wa Utawala na Menejimenti ya Rasilimali Watu CP Susan Kaganda.Picha na Jeshi la Polisi

 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Jumanne Sagini (mb) amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Camillus Wambura, kuhakikisha anasimamia kikamilifu sheria za usalama barabarani hususani katika kipindi hiki cha kuelekea mwishoni mwa mwaka.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao cha 16 cha Baraza la wafanyakazi wa Idara ya Jeshi la Polisi kilichofanyika jijini Dodoma Mhe. Sagini amesema kuwa, ni vyema wananchi wakaendelea kushirikiana na serikali kupaza sauti kukemea ajali za barabarani ambazo zimekuwa zikisababisha vifo na majeruhi.

Naye Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Camillus Wambura amesema kuwa, ili kufikia malengo ya serikali ya kuwa na Jeshi la Polisi lenye kutenda kwa nidhamu, haki, weledi na uadilifu, Jeshi limeendelea kulinda usalama wa raia na mali zao pamoja na kukabiliana na matukio na matishio mbalimbali ikiwemo uwepo wa makosa ya mmomonyoko wa maadili kwenye jamii.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.