Na.Abdulrahim Khamis.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ameyasema hayo wakati akifungua Mkutano wa Hali ya Ushirikiano wa Usalama Baharini yenye usalama ma Ustawi uliofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar-es-salaam.
Amesema Mkakati Jumuishi wa Usalama wa Bahari wa Mwaka 2050 na Kanuni, Maadili za Djibouti na Mpango wa Usalama wa Bahari ni Mifano Mizuri ya Mradi wa Usalama unaotumika katika Kanda kwa kadi kubwa.
Ameongeza kuwa Miradi ya Usalama wa Baharini imeimarisha Utawala wa Usalama Baharini wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambayo ipo mstari wa mbele kwenye Ulinzi dhidi ya matishio ya pamoja ya Usalama wa Baharini Afrika Mashariki.
Mhe. Hemed amesema Eneo la Bahari ya Jumuiya ya Afrika Mashariki limeathirika na Idadi ya vitishio vya Kiusalama Baharini ikiwemo Uhalifu, Ugaidi, urahamia, kueneza Silaha, Uvuvi haramu, uhalifu wa Mazingira ambapo Masharikiano ya Pamoja yatasaidia kumaliza matukio hayo.
Amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi imeanza kutekeleza mpango wa kuifanya Bahari kuwa ni eneo Muhimu la kukuza Uchumi wake.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema Miaka ya Karibuni kumekuwa na uvumbuzi wa utafutaji wa Mafuta na gesi katika eneo la Bahari ya Jumuiya ya Afrika Mashariki hatua hiyo inadhihirisha Usalama wa Nishati na kuongeza kuwa uvumbuzi huo unaliweka eneo la Jumuiya ya Afrika Mashariki kuwa ni eneo muhimu la usambazaji wa Nishati kwa siku zijazo.
Sambamba na hayo Mhe. Hemed ameeleza kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zitaendelea kulinda na kuboresha Miundombinu ya Bahari ikizingatiwa kuwa Bandari ya Tanzania ni moja ya Bandari zinazotoa huduma kwa Nchi mbali mbali ndani ya Afrika Mashariki.
Kwa upande wake Nakamu Mwenyekiti wa Bodi ya Kituo Cha Sera za Kimataifa Afrika (CIP) Balozi Amina Salum Ali ameeleza kuwa Asilimia kubwa ya Biashara Nchi za Afrika zinategemea Bahari pamoja na usambazaji wa Nishati mbali mbali.
Aidha amesema uwepo wa Usalama wa Bahari ni unapelekea kukuza Soko la Biashara kwa manufaa ya Baadae katika Nchi za Afrika Mashariki.
Nae Rais wa Kitui cha Sera za Kimataifa Afrika Bwana Omar mjenga amesema Tanzania ni moja kati ya Nchi zinazoshirikiana vyema na Kituo hicho ambapo ushiriki wao katika Mkutano huo ni kujadili pamoja namna ya kuiweka Bahari Salama.
Aidha amesema Nchi za Afrika zinahitaji Bahari Salama kwa lengo la kusaidia kukuza Uchumi wao na kuyaletea maendeleo Nchi hizo.
Abdulrahim Khamis
No comments:
Post a Comment