NA MWASHAMBA JUMA,
IKULU
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Al
hajj Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema uchumi wa Zanzibar umeimarika kwa nchi
kuendelea kuwa ya amani, umoja na utulivu wa watu wake.
Al hajj Dk. Mwinyi aliyasema hayo wakati akisalimiana
na wananchi na waumini wa msikiti wa Ijumaa, Masjid Nuru Muhammad kwa Mchina mwanzo
Wilaya ya Mjini Unguja, alikojumuika pamoja nao wakati wa Sala ya Ijumaa.
Al hajj Mwinyi alisema
kipindi kifupi kilichopita, Zanzibar ilipitia misukosuko ya kuyumba kwa uchumi
wake muda mchache alipoingia Madarakani mara baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar, awamu ya nane mwezi Novemba mwaka 2020.
Alisema, wakati
huo dunia ikipitia kwenye mtikisiko mkubwa wa athari za ugonjwa wa COVID 19,
hali ulioathiri zaidi uchimi wa Zanzibar, hata hivyo Dk. Mwinyi amewahakikishia
wananchi wa Visiwa vya Unguja na Pemba kwamba sasa uchumi wa nchi yao unaendea
kukua na kunawiri vizuri kadri ya amani na utulivu unavyozidi kutengemaa.
“Tulipita
kipindi kigumu, sasa hivi Alhamdullillah mwanga wa wepesi unaonekana, wakati
tunaingia madarakani ilikua katikati ya ugojwa wa COVID 19, mwezi ule hata
mishahara ilikua shida kupatikana, hali iliendelea kwasababu ugonjwa ule
uliathiri zaidi uchumi wa Zanzibar, lakini sasa kidogo kidogo hali inaendelea
kukaa sawa kwa uchumi wetu kukuwa” Dk. Mwinyi aliwaeleza wananchi hao.
Alisema kukua
kwa uchumi, kunaipa uwezo Serikali kufanya mambo mbalimbali ya maendeleo, licha
ya changamoto kadhaa za uchumi zinazoendelea kuisumbua dunia kutokana na mfumko
wa bei za bidhaa.
Alisema, licha
ya kutengemaa kwa baadhi ya sekta za maendeleo nchini, Dk. Mwinyi alieleza bado
kuna changamoto zinazosababishwa na mfumko wa bei za bidhaa ulioiathiri dunia
kukutokana na kupanda kwa gharama za maisha zilizochangiwa na kupanda kwa
uchumi wa dunia uliosababishwa na mambo mbalimbali.
“Bado changamoto
zipo sikwamba zimekwisha, sababu dunia bado haijatulia, licha ya gonjwa la
UVIKO kupungua, lakini bado kunachangamoto nyengine za kidunia zinaufanya mfumko
wa bei za bidhaa mbalimbali kuwa mkubwa, hivi sasa tunashuhudia bidhaa
zimepanda bei kwasababu ya hali ya kidunia inavyokwenda” Alieleza Al hajj
Mwinyi.
Alisema
matarajio ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwamba hali hiyo itakaa sawa na
kupata maendeleo inayoyahitaji kwa watu wake na kupunguza ukali wa maisha.
“Ndugu zangu nimesimama
hapa kukupeni moyo, nikupeni matumaini kwamba huko tunakoelekea mambo yatakaa
sawa na ugumu wa maisha utapungua In shaa Allah” Aliwaahidi wananchi hao.
Aidha, aliwaasa Wazanzibari
waendelee kuidumisha amani iliyopo ili wafaidi matunda ya utulivu wa nchi yao
kwa kushuhudia zaidi miradi mikubwa ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali ikiwemo
afya, maji, elimu na barabara.
Naye, Sheikh
Otman Maalim wakati akihutubu kwenye ibada ya sala ya Ijumaa msikitini hapo, aliwaelezea
waumini umuhimu na wajibu wa kutenda mema kwenye mambo ya haki na khairati.
Alisema kupeana salam
ni moja ya ibada kubwa kwenye na ni haki kupeana kwa uislamu nakuongeza kuwa kuirejesha
ni wajibu kwa waamini wanaposalimiwa, aidha alieleza kuitikia mialiko,
kuwarehemu wanaopiga chafya, kuwakagua
wagonjwa hospitali pamoja na kulifuata jeneza la muumini aliekufa ni miongoni
mwa haki za waumini kufanyiana kwenye mambo ya khairati.
Hata hivyo
aliwasihi waumini hao kuendelea kupeana nasaha njema na kushauriana kwenye
mambo ya kheri yenye kuleta tija kwa manufaa ya taifa.
No comments:
Post a Comment