Habari za Punde

Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa waTanga Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ambaye pia ni Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar akizungumza na wanachama wa Chama cha Mapinduzi na wananchi wa Mtae mara baada ya kuweka jiwe la msingi kituo cha afya mtae Wilaya ya Lushoto Mkoa wa Tanga  kilichopandihwa hadhi kutoka ngazi ya zahanati.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga.Mhe.Hemed Suleiman Abdulla amesema kufufuliwa kwa kiwanda cha Chai Mponde kutaimarisha uchumi wa Tanzania pamoja na kupunguza changamoto ya ajira kwa wananchi wa Mponde Wilaya ya Lushoto Mkoa wa Tanga.

Kauli hiyo imetolewa na Mlezi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga Mhe. Hemed Suleiman Abdulla alipotembelea Kiwanda hicho ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kuimarisha Chama pamoja na kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025.

 

Amesema, maamuzi ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kukifufua kiwanda hicho kilichosita kwa muda wa Miaka minane na kukikabidhi kwa mwekezaji mzawa wa Kampuni ya WCF ili kuendelea kuzalisha Chai yatasaidia kuwanufaisha wananchi wa Mponde na wa vijiji jirani.

 

Amesema kukamilika kwa kiwanda hicho kutazalisha zaidi ya ajira za kudumu na za muda mfupi ambapo ameeleza kuwa tayari muwekezaji huyo amekubali ajira zisizo za kitaalamu kuwapa kipaumbele Wakazi wa eneo hilo ili waweze kunufaika na uwepo wa kiwanda hicho katika eneo hilo.

 

Aidha Mhe. Hemed ambaye ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amefarijika kuona Kata kumi na Nne (14) kati ya Kata Kumi na Nane (18) za Wilaya hiyo zinalima Chai ambapo ni dhahiri kuwa wakazi hao watanufaika zaidi na uwepo wa kiwanda hicho.

 

Katika Ziara hiyo Mlezi huyo wa Mkoa w Tanga ameweka Jiwe la Msingi Kituo cha Afya Mtae Kata ya Mtae Wilaya ya Lushoto kilichopandishwa hadhi kutoka ngazi ya Zahanati ikiwa ni juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa.

 

Mhe. Hemed ameeleza kuwa kupandishwa hadhi kwa kituo hicho kitaweza kuwasaidia wananchi wa Mtae na maeneo jirani kuweza kupata huduma za Afya kwa urahisi. 

 

Nae Mbunge wa Jimbo la Mlalo Mhe. Rashid Abdallah Shangazi amemshukuru Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kuwa ni kiongozi wa kwanza wa kitaifa kufika eneo hilo jambo ambalo linawapata faraja wananchi wa Mtae kuona Serikali kuu inawathamini wananchi.

 

Aidha Mhe. Shangazi ameeleza kuwa hatua iliyofikia kituo hicho ni ya kuridhisha ambapo amewashukuru wananchi kwa mchango mkubwa walioutoa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.