Habari za Punde

SMZ Kuipa kipaumbele Sekta ya Elimu kwa Kuongeza Ufaulu na Kufuta Divisheni Ziro

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Ndugu Khamis Abdulla Said akizungumza na Walimu Wakuu wa Skuli za Msingi na Maandalizi Pemba kuthamini juhudi zinazofanywa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuipa kipao mbele Sekta ya Elimu kwa kuongeza ufaulu na kufuta divisheni sifuri, mkutano huo uliofanyika katika Skuli ya Maandalizi Madungu Chakechake Pemba.
Walimu wa Skuli za Msingi na Maandalizi Zanzibar wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar.Ndg. Khamis Abdallah Said wakati wa mkutano wake na Walimu uliofanyika katika ukumbi wa Skuli ya Maandalizi Madungu Chakechake Pemba. 
Walimu wa Skuli za Msingi na Maandalizi Zanzibar wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar.Ndg. Khamis Abdallah Said wakati wa mkutano wake na Walimu uliofanyika katika ukumbi wa Skuli ya Maandalizi Madungu Chakechake Pemba. 

Katibu mkuu wizara ya elimu na mafunzo ya Amali Zanzibar Ndugu Khamis Abdulla Said amewataka walimu Wakuu wa Skuli za Msingi na Maandalizi kuthamini juhudi zinazofanywa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuipa kipao mbele Sekta ya Elimu kwa kuongeza ufaulu na kufuta divisheni sifuri.

Ameyasema hayo katka Mkutano wa Kutathmini matokeo ya Mitihani ya Taifa ya Darasa la nne uliowashirikisha Walimu Wakuu wa Skuli za Msingi na Maandalizi huko katika ukumbi wa Skuli ya Maandalizi Madungu Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba.
Amesema matokeo ya mitihani ya Mwaka uliopita hayalingani na jitihada zinazowekwa katika kuimarisha Sekta ya Elimu hivyo amewataka Walimu Wakuu kujitoa kikamilifu katika kusimamia Uwajibikaji katika Skuli zao.
Aidha amesema kwa kua Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya uongozi wa Rais Dkt. Hussen Ali Mwinyi itajenga madarsa zaidi ya 2000,N yumba za walimu pamoja na Mabweni kwalengo la kuweka mazingira bora ya kufundisha na kujifunza.
Kwa upande wake Mkurugenzi Idara ya Maandalizi na Msingi Bi Fatma Mode Ramadhan akijibu hoja za Walimu Wakuu kuhusu Tathmini ya Matokeo amewataka Walimu Wakuu kuwahamadisha walimu wao kufanya Tathmini kulingana na mazingira na rasilimali walizonazo.
Akifafanua zaidi amesema si vyema kuacha kuwapima wanafunzi kwasababu Skuli haina Mashine ya kutolea fotokopi na badala yake chaki na ubao zinaweza kutumika kuwapima Wanafunzi hao.
Aidha amesema Wanafunzi wa Maandalizi nirahisi mno kuwapima kwani upimaji wao unajikita katika maneno matatu ambayo ni Kusoma ,Kuandika,na Kuhesabu.
Wakati huohuo Bifatma amewataka Walimu Wakuu kutoa Mashirikiano ya kutosha kwa wazazi ili kubaini changamoto zinazowakabili watoto na kuweza kuzitatua.
Akiitoa ushauri wake Mwalimu Mkuu Skuli ya Kisiwa Panza Nd. Fatawi Mselemu Juma amesema ufaulu wa Wanafunzi katika kila Skuli Unawezekana iwapo Walimu , Wazazi na Kamati watatoa mashirukiano ya kutosha
Akifafanua zaidi Mwalimu Fatawi amewataka Walimu kuweka Utaratibu wa kuwashajihisha watoto kwa kuwapa Zawadi ndogo ndogo kwa lengo la kuwatengezea hamu na ari ya kujifunza.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.