Habari za Punde

Mtandao wa Jeshi la Polisi Wanawake TANZANIA (TPF-NET) Wameshiriki Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Jijini Dodoma


Na. Benedict Mlawa wa Jeshi la Polisi

Jeshi la Polisi  kupitia Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania (TPF-NET)  limeshiriki katika kuadhimisha sherehe ya siku ya Wanawake  Duniani  iliyofanyika Machi  08, 2023 Wilayani  Kondoa Jijini Dodoma.

Maadimisho hayo yameongozwa na  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma  Mhe. Rosemary Senyamule leo Machi 08, 2023  ambaye  ameongoza  viogozi wa Kiserikali, Chama, Vyombo vya Ulinzi na Usalam, Taasisi , Mashirika, Dini  Pamoja na Wananchi  katika kuadhimisha ya siku ya Wanawake Duniani  ambayo imefanyika  kimkoa  Wilaya  ya Kondoa Jijini Dodoma,  ambapo maadhimisho haya yamebebwa na kauli mbiu isemayo “Ubunifu na Mabadiliko ya Technolojia, chachu katika kuleta Usawa wa Kijinsia”

Mkuu wa Mkoa aliwashukuru na kuwapongeza viongozi na wakazi wa Wilaya ya Kondoa kwa maandalizi mazuri  waliyoyafanya  kwa  kuupokea ugeni mzima wa mkoa wa Dodoma  katika wilaya yao.

Pia, Senyamule alisema anamshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.  Daktari Samia Suluhu Hassan kwa kuwa chachu ya mafanikio kwa Wanawake hapa  nchini kwa kuamini kwamba Wanawake wanaweza  hata ukiangalia katika  uteuzi wake waviongozi  wanawake wamepewa nafasi kwa kuamini  usawa wa Kijinsia.

Hata hivyo,  Mkuu wa Mkoa Rosemary Senyamule aliwa taka wanawake kujitokeza na kuzifanyia kazi fulsa mbalimbali ambazo  zinatolewa serikali  ili kuweza kufikia malengo ya Usawa wa Kijinsia kwa maendeleo endelevu.

Pia,  Mkuu wa Mkoa Rosemary Senyamule aliongeza kwa kusema Jamii lazima izingatie haki za watoto wa kike kwa  kumlinda mtoto wa kike dhidi ya ndoa za utotoni  ili aweze  kufikia na kufaidi huduma za jamii ikiwa  ni  pamoja na kupata elimu yenye kuwezesha kudai na kumlinda mtoto wa kike dhidi ya Ukatili wa Kijia.

Sambamba na hayo Mkuu wa Mkoa Rosemary Senyamule aliwatunuku zawadi wanafunzi  mbalimbali wa Wilaya zote za Jiji la Dodoma waliofanya vizuri kwa kupata ufaulu  wa (DIVISION 1)  katika mitihani yao ya  Mwisho  ya  kidato cha nne mwaka 2022.


 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.