Habari za Punde

Rais Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan akabidhi Bure Hati za Viwanja kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) EREA, EABC na EALS Mkoani Arusha

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Dkt. Peter Mathuki Hati ya Umiliki wa Ardhi yenye ukubwa wa ekari 125 bure bila malipo yoyote kwa ajili ya Jumuiya hiyo mara baada ya mazungumzo yaliyofanyika Ikulu Ndogo ya Arusha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Biashara la Afrika Mashariki (EABC) John Bosco Kalisa Hati ya umiliki wa Ardhi yenye ukubwa wa ekari 3 bure bila malipo yoyote kwa ajili ya Baraza hilo Jijini Arusha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Mwanachama Mkazi wa Baraza la Chama cha Wanasheria wa Afrika Mashariki (EALS) Moses Mahuna Hati ya umiliki wa Ardhi yenye ukubwa wa ekari 5 bure kwa ajili ya matumizi ya Chama hicho cha Wanasheria kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu Ndogo ya Arusha 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Katibu Mtendaji wa Chama cha Udhibiti wa Nishati kwa Afrika Mashariki Geoffrey Mabea Hati ya umiliki wa Ardhi yenye ukubwa wa ekari 4 kwa ajili ya matumizi ya Chama hicho katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Ndogo ya Arusha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Dkt. Peter Mathuki wanne kutoka (kushoto), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax watano kutoka (kulia), Mwakilishi kutoka Chama cha Wanasheria wa Afrika Mashariki (EALS) Moses Mahuna watatu kutoka (kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Biashara la Afrika Mashariki (EABC) John Bosco Kalisa wanne kutoka (kulia), Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella watatu kutoka (kulia) pamoja na Katibu Mtendaji wa Chama cha Udhibiti wa Nishati kwa Afrika Mashariki Geoffrey Mabea wa kwanza (kulia) kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu Ndogo ya Arusha 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Waziri wa mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax pamoja na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Balozi Mbarouk Nassoro Mbarouk mara baada ya kukabidhi Hati ya Umiliki wa Ardhi kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) katika Ikulu Ndogo ya Arusha

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella mara baada ya kukabidhi Hati ya Umiliki wa Ardhi kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) katika Ikulu Ndogo ya Arusha tarehe 03 Machi, 2023.

PICHA NA IKULU.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.