Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akikabidhi majiko banifu 114 yanayotumia nishati safi na Salama ya kupikia katika hafla iliyofanyika Wilaya ya Bahi Kijiji cha Zanka na Kigwe wamenufaika. Majiko hayo yametolewa na jumuiya ya wanawake ya wakala wa Nishati Vijijini ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani. Wengine katika picha ni Mkuu wa Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mhe. Godwin Gondwe.
Sehemu ya wananchi wa Wilaya ya Bahi Kijiji cha Zanka na Kigwe wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma
Mhe. Rosemary Senyamule (Hayupo pichani) katika halfa ya ugawaji Majiko banifu yametolewa
na jumuiya ya wanawake ya wakala wa Nishati Vijijini ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani.
Akizungumza na wananchi wa vijiji hivyo, Senyamule
amesema kuwa Matumizi ya kuni na Mkaa yamekuwa chanzo kikuu kinachotumika kwa
kupikia hususani Maeneo ya Vijijini na kupelekea kutumika kwa kiwango kikubwa
na hivyo kuleta athari katika mazingira.
“Serikali itaendelea kuweka vivutio kwa wazalishaji na
wasambazaji wa Teknolojia na bidhaa za nishati safi na salama ya kupikia na
kuongeza wigo wa upatikanaji wa bidhaa pamoja na kutoa unafuu wa gharama ili
kuwezesha watumiaji kutumia bidhaa hiyo” Alisisitiza Mhe. Senyamule.
Zaidi ya tani milioni mbili za Mkaa zimekuwa zikitumika
kwa mwaka kama nishati ya kupikia hivyo imeleta athari za mazingira na afya
katika jamii, zaidi ya asilimia 85 ya kaya hapa nchini hutumia kuni na Mkaa
kama chanzo kikuu cha nishati ya kupikia.
Naye Mkurugenzi Uendelezaji Masoko na Teknolojia Wakala
wa Nishati Vijijini (REA) Bi. Advera Mwijage amesema jiko linatumia nishati
mbili ambayo ni jiko la kuni na mkaa ambalo linaweza kutumika sehemu yoyote na
inamsaidia mwananchi au mama wa kitanzania kupunguza gharama ya matumizi ya
fedha na kupunguza ukataji wa miti ovyo.
Vilevile wenyekiti wa kijiji cha Kigwe Jeremia E.Sobayi amesema
kila mwananchi anatakiwa kuwa balozi
mzuri katika matumizi sahihi ya majiko hayo na kila mmoja wao awe mlinzi
wa mwenzake ili isije kutokea mtu akafanyia matumizi mengine nje ya malengo
yaliyowekwa ya kutunza mazingira kwa kutokukata miti hovyo.
No comments:
Post a Comment