Habari za Punde

Wananchi wajengewe uelewa juu ya Baraza la ushindani halali wa Biashara Zanzibar

Mrajisi Baraza la ushindani halali wa Biashara Zanzibar Fatma Gharib Haji  akizungumza na wanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya Biashara wakati alipokua akifungua kongamano la kuwajengea uwezo Wanafunzi kulitambua  Baraza hilo ikiwa ni shamrashamra kuelekea maashimisho ya siku ya   kumlinda mtumiaji  Duniani ambayo huadhimishwa Kila ifikapo tarehe 15 machi, Kitaifa yataadhimishwa Mkoani  Mwanza yakiwa na kauli mbiu “kumjengea uwezo mtumiaji katika matumizi ya nishati na nishati mbadala” ,hafla iliyofanyika Skuli ya Sekondari ya Biashara Mombasa Zanzibar.Machi 10 2023.

PICHA NA FAUZIA MUSSA –MAELEZO ZANZIBAR.

Mkurugenzi huduma za Baraza la  ushindani halali wa Biashara Zanzibar Fatma Ali yahya akiwasilisha mada ya muundo wa Baraza wakati wa kongamano la kuwajengea uwezo Wanafunzi kulitambua  Baraza hilo ikiwa ni shamrashamra kuelekea maashimisho ya siku ya   kumlinda mtumiaji  Duniani ambayo huadhimishwa Kila ifikapo tarehe 15 machi ,Kitaifa yataadhimishwa Mkoani  Mwanza yakiwa na kauli mbiu “kumjengea uwezo mtumiaji katika matumizi ya nishati na nishati mbadala” hafla iliyofanyika Skuli ya Sekondari ya Biashara Mombasa Zanzibar.Machi 10 2023.

PICHA NA FAUZIA MUSSA –MAELEZO ZANZIBAR.

Afisa Sheria mwandamizi Thneyuu Mbarouk akiwasilisha mada ya utaratibu na muongozo wa Rufaa wakati wa kongamano la kuwajengea uwezo Wanafunzi kulitambua  Baraza la  ushindani halali wa Biashara ikiwa ni shamrashamra kuelekea maashimisho ya siku ya   kumlinda mtumiaji  Duniani ambayo huadhimishwa Kila ifikapo tarehe 15 machi ,Kitaifa yataadhimishwa Mkoani  Mwanza yakiwa na kauli mbiu “kumjengea uwezo mtumiaji katika matumizi ya nishati na nishati mbadala” hafla iliyofanyika Skuli ya Sekondari ya Biashara Mombasa Zanzibar.Machi 10 2023.PICHA NA FAUZIA MUSSA –MAELEZO ZANZIBAR.

Mwanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya Biashara  Sumayya Haji Khamis akiuliza suali wakati wa kongamano la kuwajengea uwezo Wanafunzi kulitambua  Baraza  Baraza la  ushindani halali wa Biashara   ikiwa ni shamrashamra kuelekea maashimisho ya siku ya   kumlinda mtumiaji  Duniani ambayo huadhimishwa Kila ifikapo tarehe 15 machi ,Kitaifa yataadhimishwa Mkoani  Mwanza yakiwa na kauli mbiu “kumjengea uwezo mtumiaji katika matumizi ya nishati na nishati mbadala” hafla iliyofanyika Skuli ya Sekondari ya Biashara Mombasa Zanzibar.Machi 10 2023.

PICHA NA FAUZIA MUSSA –MAELEZO ZANZIBAR.

Mwanafunzi Skuli ya Sekondari ya Biashara  Alfred Jeremiah Robert form akichangia mada ya muundo wa Baraza kwenye kongamano la kuwajengea uwezo Wanafunzi kulitambua  Baraza  Baraza la  ushindani halali wa Biashara   ikiwa ni shamrashamra kuelekea maashimisho ya siku ya   kumlinda mtumiaji  Duniani ambayo huadhimishwa Kila ifikapo tarehe 15 machi ,Kitaifa yataadhimishwa Mkoani  Mwanza yakiwa na kauli mbiu “kumjengea uwezo mtumiaji katika matumizi ya nishati na nishati mbadala” hafla iliyofanyika Skuli ya Sekondari ya Biashara Mombasa Zanzibar.Machi 10 2023.PICHA NA FAUZIA MUSSA –MAELEZO ZANZIBAR.
Mwanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya Biashara  Khadija Hassan Omar akichangia mada ya utaratibu na muongozo wa Rufaa kwenye kongamano la kuwajengea uwezo Wanafunzi kulitambua  Baraza  Baraza la  ushindani halali wa Biashara   ikiwa ni shamrashamra kuelekea maadhimisho ya siku ya   kumlinda mtumiaji  Duniani ambayo huadhimishwa Kila ifikapo tarehe 15 machi ,Kitaifa yataadhimishwa Mkoani  Mwanza yakiwa na kauli mbiu “kumjengea uwezo mtumiaji katika matumizi ya nishati na nishati mbadala” hafla iliyofanyika Skuli ya Sekondari ya Biashara Mombasa Zanzibar.Machi 10 2023.PICHA NA FAUZIA MUSSA –MAELEZO ZANZIBAR.
Mwanafunzi Skuli ya Sekondari ya Biashara Hemed Ali Hemed akiuliza suali wakati wa kongamano la kuwajengea uwezo Wanafunzi kulitambua  Baraza  Baraza la  ushindani halali wa Biashara   ikiwa ni shamrashamra kuelekea maashimisho ya siku ya   kumlinda mtumiaji  Duniani ambayo huadhimishwa Kila ifikapo tarehe 15 machi ,Kitaifa yataadhimishwa Mkoani  Mwanza yakiwa na kauli mbiu “kumjengea uwezo mtumiaji katika matumizi ya nishati na nishati mbadala” hafla iliyofanyika Skuli ya Sekondari ya Biashara Mombasa Zanzibar. Machi 10 2023. PICHA NA FAUZIA MUSSA –MAELEZO ZANZIBAR. 
 

Na Rahma Khamis Maelezo                   

Baraza la Ushindani Halali la Biashara Zanzibar limeitaka jamii kuwa makini katika kununua bidhaa wanazotumia ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza.

Hayo yameelezwa na Mrajisi wa Baraza hilo Fatma Gharib Haji katika Skuli ya Biashara Mombasa wakati alipokua akifungua kongamano la kuwajengea uwezo wanafunzi kuhusu kulitambua baraza la Ushindani Halali la Biashara ikiwa ni shamrashamra za kuelekea maadhimisho ya siku ya kumlinda mtumiaji.

Amesema kuna baadhi ya wafanya biashara bidhaa zao haziko salama jambo ambalo linaweza kupelekea madhara kwa watumiaji   wa chakula.

Aidha amefahamisha kuwa Taasisi zote za Serekali zinazoshuhulikia bidhaa zinahakikisha kuwa zinamlinda mtumiaji na maslahi yake kwa kuzingatia sheria na taratibu zake.  

Mrajis amefafanua kuwa lengo la kongamano hilo ni kuifahamisha jamii kuhusiana na  maadhimisho hayo, ambayo yanatarajiwa kufanyika Mwanza kitaifa Mach 15 mwezi huu.

 Mkurugenzi wa Baraza hilo Fatma Ali Yahya Akitoa Mada ya Mundo wa Baraza  amefafanua  kuwa Baraza lina jukumu la kusikiliza malalamiko kwa Watumiaji wa biashara na kutoa maamuzi pamoja na kutunza kumbkumbu ili kuhifadhi taarifa za mlalamikaji.

Nae Afisa Sheria Mwandamizi Thneyuu Mbarouk Hassan amesema kuwa Baraza huangalia mfumo wa ushindani na udhibiti wa masoko ili kuhakikisha inalindwa  Afya ya Watumiaji.

Amefahamisha kuwa mtu yeyete ambae amefanyiwa kinyume na utaratibu katika udhibiti wa bidhaa ana haki ya kupeleka malalamiko yake katika taasisi husika na endapo hakuridhika ana haki ya kufika baraza la Ushindani kwa ufafanuzi zaidi.

Aidha ameeleza kuwa endapo mlalamikaji atapeleka mashauri (kesi) kwa ajili ya uchambuzi wa mashauri hayo basi atachukuliwa hatua kwa zaidi  ikiwemo haki ya rufaa.

Nao washiriki wa kongamano hilo wamelishukuru Baraza kwa kuwapatia elimu hiyo na kuahidi kuyafanyia kazi waliopatiwa kwa wanafunzi wenzao na jamii kwa ujumla.

Katika kongamano hilo mada mbili zimejadiliwa ikiwemo Mfumo wa Baraza, Utaratibu na Muongozo wa Rufaa ambapo Kaulimbiu ya mwaka huu KUMJENGEA ULINZI MTUMIAJI KATIKA MATUMIZI YA NISHATI NA NISHATI MBADALA

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.