Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu Jamal Kassim Ali akijumuika na Viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali pamoja na wanafamilia katika Dua ya kumuombea Mhe,Hafidh Suleiman Almasi Ikiwa ni muendelezo wa Maadhimisho ya kuwaenzi Viongozi wa Kitaifa ,Waasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar hafla iliofanyika Kijijini kwao Kinduni Kichungwani kaskazini Unguja.
Baadhi ya Wananchi mbalimbali waliohudhuria katika hafla ya kumuombea Dua Mhe,Hafidh Suleiman Almasi Ikiwa ni muendelezo wa Maadhimisho ya kuwaenzi Viongozi wa Kitaifa ,Waasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar hafla iliofanyika Kijijini kwao Kinduni Kichungwani kaskazini Unguja.
|
Waziri wa Nchi, Afisi ya Rais, Ikulu Mheshimiwa Jamal Kassim Ali amesema mchango wa Viongozi Waandamizi waliyojitoa muhanga kugombania nchi ili kuhakikisha uhuru unapatikana iko haja ya kuwaenzi na kuwakumbuka kutokana na juhudi walizozifanya.
Hayo ameyasema huko Kinduni Kichukwani, Wilaya ya Kaskazini ‘B’ Unguja wakati wa hafla ya kufanya ziara na kusoma dua katika Kaburi la Marehemu Hafidhi Suleiman Almas
Amesema viongozi hao wametoa mchango mkubwa katika kupambana na kugombania uhuru wa taifa lao kwa hali na mali hadi kufikia kujivunia matunda na maendeleo nchini.
Ameeleza kuwa viongozi hao waliotangulia mbele ya haki wameweka historia nzuri isiyosahaulika nchini na kuacha kumbukumbu kwa vizazi vilivyopo na vijavyo.
Nae Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mheshimiwa Ayoub Mohamed Mahamud amesema Shughuli hiyo ya ziara na Kisomo cha dua imeasisiwa mwaka jana kwa hapa Zanzibar mwanzo kulikuwa na Siku ya Mashujaa ya kuwaenzi na kuwakumbuka viongozi wa kitaifa.
“Ni dhahiri kwamba nia ya Serikali ni njema ya kutoa dua kwa viongozi wa kitaifa ya kuwaenzi waasisi hao hivyo iko haja ya kuwaombea dua” alifahamisha Mkuu wa Mkoa huyo.
Kwa upande wa Kiongozi wa Familia Iddi Hafidh Suleiman (Sancho) amewashukuru viongozi waliopanga mpango huo wa dua kwa Marehemu pamoja na walioshirikiana kufanikisha hafla hiyo
Ameomba kuwepo na mashirikiano ya pamoja kwa familia na wajane wa Marehemu hao ambao walijitoa muhanga kuhakikisha wanapata uhuru wa nchi yao
Dua hiyo imeongozwa na Sheikh Suleiman Simai Ali kutoka Ofisi ya Mufti Zanzibar kwa kushirikiana na Viongozi mbali mbali wa Chama na Serikali pamoja na wanafamilia ,
No comments:
Post a Comment