Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo
akitoa maelekezo wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua na kutatua changamoto
zinazowakabili wananchi wanaozungukwa na mradi wa uzalishaji kokoto katika
Kijiji cha Mundemu Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya Bahi
Godwin Gondwe.
Eneo
ambalo mradi wa uzalishaji kokoto katika Kijiji cha Mundemu Wilaya ya Bahi mkoani
Dodoma unafanyika na kulalamikiwa na wananchi kuleta changamoto ya kusambaa kwa
vumbi.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo
akisindikizwa na Mkuu wa Wilaya Bahi Godwin Gondwe kuelekea kwenye gari
kwa ajili ya kuanza ziara ya kukagua na kutatua changamoto zinazowakabili wananchi
wanaozungukwa na mradi wa uzalishaji kokoto katika Kijiji cha Mundemu Wilaya ya
Bahi mkoani Dodoma.
Pia
ametoa muda huo kwa wawekezaji hao kuhakikisha wananchi hao wanalipwa fidia ili
waweze kuondoka na kupisha mradi huo vinginevyo utasitishwa kuendelea na
shughuli zake.
Dkt.
Jafo ametoa maagizo hayo Aprili 04, 2023 wakati wa ziara ya kikazi kwa lengo kukagua
na kujioenea hali halisi, kujadili hatua stahiki zinazofaa kutatua changamoto
zinazowakabili wananchi wanaozungukwa na mradi huo.
Akziungumza
wakati wa ziara hiyo amesema kuwa Serikali inathamini uwekezaji unaofanywa hapa nchini
lakini haitavumilia kuona wananchi wawekezaji wanakiuka sheria ya mazingira
hivyo wananchi kupapata madhara.
“Nimepata
malalamiko mengi kutoka kwa wananchi wakililamika kupata vumbi kutokana na shughuli
inayofanyika hapa na tume iliundwa hapa na watu wa madini na kutoa maelekezo
lakini hawakufuata sasa hatuwezi kuvumilia watu hawa hawafuati sharia za nchi,
maelezo yangu ni hayo mawili vingine mradi huu utafungwa,” alisisitiza.
Hivyo,
kutokana na malalamiki ya wananchi kuhusu milipuko ya barudi wakati wa kuoasua
miamba alisema hilo liko chini ya sekta ya madini hivyo alitoa wito kwa
wataalamu wa madini kufika na kufuatilia changamotio hiyo.
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Bahi Godwin Gondwe alisema alimshukuru Waziri Jafo
kwa kufika katika eneo hilo na kusikiliza na kushughulikia changamoto hizo.
Aliahidi
kuyasimamia maelekezo aliyotoa ili na kuhakikisha wawekezaji hao wanatekeleza
maelekezo hayo ndani ya siku 45 ambazo Waziri Jafo ametoa ili kuhakikisha
madhara ya vumbi hayawafikii wananchi.
Awali
baadhi ya wananchi wa kijiji hicho wakiwemo Diwani wa Kata ya Mundemu Stanley
Mtati, Bw. Richard Nyagani walisema wamekuwa wakipata kero ya milipuko
inayotumika kulipua mawe ambayo inaletea madhara yakiwemo kuharibika kwa
nyumba.
Hivi
karibuni Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)- Kanda ya
Kati kwa kushirikiana na Ofisi ya Afisa Madini Mkazi – Dodoma na Ofisi ya
Mkurugenzi wa Wilaya ya Bahi ilifanya Ukaguzi katika eneo la mradi huo.
No comments:
Post a Comment