Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Mwinyi Amejumuika na Wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Katika Iftari

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimkaribisha iftari Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh. Saleh Omar Kabi tende wakati wa Iftari Maalumu aliyowaandaliwa Wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja iliyofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Amali Mkokotoni Unguja.   
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja(hawako pichani) katika Iftari Maalum aliyowaandalia iliyofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Amali Mkokotoni Wilaya ya Kaskazini "B" Unguja, (kulia kwa Rais) Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi na (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Sheria,Katiba, Utumishi na Utawala Bora Zanzibar Mhe. Haroun Ali Suleiman. 






Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe.Ayoub Mohammed Mahmoud (kushoto kwa Rais) akitowa maelezo ya zawadi ya futari iliyotolewa na Makundi Maalum ya Wananchi wa Mkoa huo, baada ya kumalizika kwa Iftari aliyowaandaliwa katika ukumbi wa Chuo cha Amali Mkokotoni Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana Mwakilishi wa Makundi Maalumu Mkoa wa Kaskazini Unguja Ndg.Khamis Khamis Haji,baada ya kukabidhiwa zawadi ya Futari, baada ya kumalizika kwa Iftari Maalum aliyowaandalia katika ukumbi wa Chuo cha Amali Mkokotoni Wilaya ya Kaskazini "B" Unguja. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kutoa shukrani kwa Wawakilishi wa Makundi Maalum ya  Mkoa wa Kaskazini Unguja baada ya kukabidhiwa futari, baada ya kumalizika kwa Iftari maalum aliyowaandalia katika ukumbi wa Chuo cha Amali Mkokotoni Wilaya ya Kaskazini "B" Unguja.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.