SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema imejikiza zaidi
kwenye teknolojia ya kisasa ili kuboresha sekta ya utalii kwa kuimarisha
miundominu ya kisasa ya utoaji huduma bora kupitia viwanja vya ndege vya
Zanzibar ili kuwavutia watalii wengi zaidi kutoka mataifa mbambali ya dunia
wanaoitembelea Zanzibar ili wakirudi kwao wawe mabalozi wazuri wakusimulia
mazuri yanayopatikana kwenye visiwa vya Unguja na Pemba na Tanzaia kwa ujumla.
Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi ameyasema
hayo alipozungumza na Balozi wa Ubelgiji nchini Tanzania, Mhe. Peter
Huyghebaert, Ikulu Zanzibar aliefika kujitambulisha.
Dk. Mwinyi, alimueleza
balozi huyo kwamba Zanzibar utalii ndio sekta mama ya uchumi ambao inahusisha
na sekta nyengine za uwekezaji kupitia sera yake ya uchumi wa Buluu.
Rais Mwinyi
alisema Uhusiano uliopo baina ya Ubelgiji na Tanzania ikiwemo Zanzibar kumekuwa
na urafiki mzuri baina yao kwani nchi imekuwa ikipokea watalii wengi kutoka
huko.
Alisema kupitia
sekta ya utalii kumekuwa na safari za ndege za moja kwa moja kutoka Ubelgiji
hadi Zanzibar na kumueleza balozi huyo uhusiano uliopo baina ya pande mbili
hizo anaamini wataalii zaidi wataongezeka katika kuimarisha urafiki wao.
“Zanzibar tuna
safari za ndege za moja kwa moja kutoka Ubegiji, hali hii pia imeongeza watalii
wengi kutoka huko, tunaamini idadi itaongezeka zaidi kutokana uhusiano mzuri
baina yetu” alisifu, Dk. Mwinyi.
Akizungumzia
sekta ya Afya Rais Dk. aliueleza balozi huyo kuangalia uwezekano wakuimarisha
ushirikiano zaidi kwenye sekta hiyo hasa masuala ya TEHAMA ambako eneo hilo
lina uhitaji zaidi ili kuongeza ujuzi na kubadilishana uzoefu kwa wafanyakazi
na wahudumu wa fani hiyo kupitia taasisi ya Karume amako vijana wengi huchukua fani ya Afya.
Pia Rais Dk.
Mwinyi alimueleza Balozi Huyghebaert ikiwa Ubelgiji ni mwanachama wa Umoja wa
Ulaya (EU) yenye miradi mingi ya maendeleo kuangalia zaidi fursa zilizopo kupitia
ushirikiano wa diplomasia uliopo baina ya Ubelgiji na Tanzania ikiwemo Zanzibar
kunufaika na fursa zilizopo huko na uwezekano wa kuzifikia katika kuimarisha
zaidi uhusino baina yao.
Kwa upande wake
Bolozi Peter Huyghebaert, aliishurkuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na
kumpongera Rais Dk. Mwinyi kwa juhudi zake za kuiletea maendeleo Zanzibar.
Alisema urafiki
wa diplomasia uliopo baina ya Ubelgiji na Tanzania ikiwemo Zanzibar anaamini
utaendelea kuzaa matunda mazuri yatakayowanufaisha wananchi wa pande mbili
hizo.
Alisema Ubelgiji
imekua ikishirikiana zaidi na Afika kupitia miradi mbalimbali ya maendeleo kwa
sekta zote za taasisi za umma na binafsi.
Alimueleza Rais
Dk. Mwinyi kwamba hadi sasa Ubelgiji inaendeleza miradi mbalimbali kwenye kanda
tano za Afrika, Tanznia ikiwa miongoni mwao kwa kuyafikia maeneo mengi hasa
kwenye sekta mtandao ikiwemo kushirikina katika masuala ya Afya mtandao ambako Ubekgiji
na Tanzania wanashirikiana kwenye matumizi ya teknolojia ya kisasa kuangalia
uwezekano wa kunusuru vifo vya watoto kabla ya kuzaliwa, aidha, masuala ya
huduma za pasi mtandao ambako Ubelgiji inashirikiana na Idara ya uhamiaji na
sekta nyengine kwenye ustawi wa maendeleo ukiwemo mradi wa “wanawake wanaweza” katika kuwainua wanawake kuendana na
maadiliko chanya ya maendeo na kujikwamua kiuchumi kupitia taasisi za serikali
na asasi za kiraia.
Pia balozi huyo alimuahidi Dk. Mwinyi kushirikiana kwenye
maeneo mbalimbali ya maendeleo ikiwemo kuimarisha matumizi ya IT na teknolojia hasa
kwenye sekta ya afya kwa kuimarisha huduma za Afya mtandao pamoja na kuangalia
fursa zilizopo kupitia uchumi wa buluu jinsi ya kuwanufaisha wananchi wa pande mbili
hizo katika kuendeleza uhusiano wa kirafiki uliopo baina yao.
Tanzania na Ubelgiji zimekua na uhusiano wa diplomasia na
biashara tangu miaka ya 1980 ambapo kwa
mara ya kwanza Ubelgiji ilifungua ubalozi wake Dar es Salaam mwaka huo na Tanzania
ilifungua ubalozi wake mji mkuu wa nchi hiyo, Brussels ambako balozi wa
Tanzania nchini humo ni Mhe. Jestas Abouk Nyamanga tangu mwaka 2019
IDARA YA MAWASILINO, IKULU ZANZIBAR.
No comments:
Post a Comment