IMEELEZWA kwamba suala la kuwepo
Utawala Bora katika nchi sio sera madhubuti na kanuni nzuri pekee, bali ni kunahitajika kuwepo ufanisi kwenye utoaji
na ufikishaji wa huduma kwa wananchi pamoja na utawala maridhawa wa
rasilimali za umma nchini.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa
Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, ameeleza hayo huko hotel ya Golden tulip
mjini Zanzibar aliposoma hotuba kwa niaba ya rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Mwinyi alipomuwakilisha kwenye ufunguzi wa
Jukwa la Mkutano wa Pili wa Sekta ya Umma na Wakaguzi wa Ndani Tanzania.
Mhe. Dk Mwinyi amesema kwamba hivi
sasa Tanzania inashuhudia mabadiliko makubwa kutokana na msukumo wa
jamii, na kulazimika kuongezeka uwazi
katika matumizi ya fedha za umma na kwamba hatua hiyo inahitaji Kamati , Bodi ,
Maafisa Masuuli na Wakaguzi wa ndani
kujipanga vyema ili kuwezesha mageuzi
kwenye muelekeo wa ufikishaji huduma katika kuenua maisha ya watu nchini.
Aidha amefahamisha kwamba mkutano
huo utatoa fursa kwa wadau wa Ukaguzi na
Utawala kubadilishana mawazo na uzoefu
juu yambinu bora zitakazosaidia kuleta
mageuzi ya kiutawala kwenye taasisi zote za umma na binafasi na kutoa muono wa , mbinu na
mikakati sahihi yakufikia lengo la
mageuzi kwenye sekta ya umma kwa maslahi
ya wananchi.
Sambamba na hayo Dk. Mwinyi amesema
kwamba ni muda muafaka sasa wa kukabiliana na changamoto mbali mbali zikiwemo za kimiundo ya taasisi na kuondokana na muelekeo
uliozoeleka wa kusimamia na kutenda kazi kwa kutoendana na mahitaji ya wakati
uliopo.
Mhe. Dk. Mwinyi emefahamisha kwamba
ni jambo muhimu katika kukidhi haja ya matarajio ya wananchi yakuleta mageuzi kwa taasisi hizo
kujipanga upya katika ufikishaji wa huduma bora kwa umma kwa kukuza ufanisi na
kupata matokeo yanayoendana na matarajio ya watanzania.
Amesema kwamba wakaguzi wa ndani
ndio jicho na masikio ya sekta ya umma nchini
na kwamba serikali za Tanzania zinaendelea kujidhatiti katika uimarishaji na
kuweka umakini wa shughuli za ukaguzi wa
ndani katika kuleta ufanisi zaidi kukidhi matarajio ya wananchi kimaendeleo.
Hata hivyo Dk. Mwinyi emesema
kwamba wakaguzi wamekuwa wakifanya kazi kubwa
bila kuchoka kuwezesha ofisi hizo kufikia malengo ingawa wapo baadhi ya
wengine ambao hawajaelewa madhumuni ya kuwepo kwao kwenye ofisi hizo kwa
makusudi ama kutokujijua na kuwataka kubadilika kwa kuondokana na mwenendo huo.
Aidha Dk Mwinyi ameonya kwamba
serikali haitakuwa na ustahamilivu kwa wakaguzi wa ndani wasiotimiza wajibu wao
ipasavyo na kuwataka watumishi hao wote kufanyakazi kwa bidii na kuzingatia maadili ya kazi zao, matakwa na
vigezo vya kitaaluma.
Mapema Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa
Zanzibar Bi Fatma Mohammed, amesema kwamba uwajibikaji wa wakaguzi wa ndani ni
muhimu kwa matumizi sahihi ya rasilimali za umma na kwamba mkutano huo
utasaidia kuchangia kuwepo mabadiliko ya kiutendaji yanayohitajika licha ya
kuwepo changamoto mbali mbali kwenye kada hiyo.
Hata hivyo, Mkaguzi huyo wa ndani amebainisha
kuwepo changamoto mbali katika sekta hiyo ikiwemo kutokuwepo sheria makhusisi
inayosimamia masuala ya ukaguzi wa ndani, upungufu wa utaalamu wa kileo hasa
katika masuala yanayohgusu ukaguzi wa
utaalamu wa teknolojia na kwamba kwamba serikali kupitia ofisi yake inafanya
juhudi kubwa kutatua changamoto hizo.
Mkutano huo wa siku mbili
unawashiriki wanataaluma, wakaguzi na viongozi wa taasisi mbali mbali
zinazosimamia masuala ya ukaguzi wa ndani kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.
Imetolewa na ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kupitia Kitengo chake Cha Habari leo tarehe 24.04.03
No comments:
Post a Comment