Habari za Punde

Mama Mariam Mwinyi Amekutana na Binti wa Mtawala wa Zamani wa Qatar

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundatiom amekutana na kuzungumza na Binti wa Mtawala wa zamani wa Qatar Sheikha Alanoud Hamad Al-Thani jijini Doha, Qatar. 

Katika kikao hicho kwa pamoja walibadilishana mawazo juu ya ustawi wa wanawake na vijana hususan wanawake katika kujiendeleza kiuchumi, afya na elimu.

Sheikha amempongeza mama Mariam Mwinyi kwa kuanzisha Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation ambayo imekuwa inapambana na unyanyasaji na ukatili wa kijinsia pamoja na kumwezesha mtoto wa kike katika masuala ya afya ya uzazi, kuwawezesha pia wanawake wanaojishughulisha na ukulima wa mwani.


Mama Mariam Mwinyi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora amekutana na  Binti wa mtawala wa zamani wa Qatar Sheikha Alanoud Hamad Al-Thani jijini Doha, Qatar. 

Katika kikao hicho kwa pamoja walibadilishana mawazo juu ya ustawi wa wanawake na vijana hususan wanawake katika kujiendeleza kiuchumi, afya na elimu.

Sheikha amempongeza mama Mariam Mwinyi kwa kuanzisha Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora ambayo imekuwa inapambana na unyanyasaji na ukatili wa kijinsia pamoja na kumwezesha mtoto wa kike katika masuala ya afya ya uzazi, kuwawezesha pia wanawake wanaojishughulisha na ukulima wa mwani.

📆 22 Mei 2023

📍Doha, Qatar

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.