Habari za Punde

Mama Mariam Mwinyi Amewataka WanaDiaspora Wanawake Kuenbdeleza Utaratibu Wao Kuwasaidia Wanawake Zanzibar

Mke wa Rais Zanzibar Mama Mariam Mwinyi amewasihi WanaDiaspora wanawake waishio nchini Qatar kuendeleza utaratibu wao wa kuleta mchango na shukrani nyumbani. Amebainisha umuhimu wa kuwasaidia wanawake Zanzibar.

Mama Mariam Mwinyi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora, alitumia nafasi hiyo kuwahutubia WanaDiaspora wanawake walioko Qatar wakati wa sherehe za kutimiza mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwa taasisi yake. Sherehe hizo zilifanyika jana tarehe: 22 Mei 2023, Doha, Qatar 

Mama Mariam Mwinyi ametoa wito kwa wanawake  hususan WanaDiaspora waishio Qatar, kuwa makini katika malezi ya watoto. Hii ni kufuatia kuongezeka kwa kasi kwa wimbi la udhalilishaji, ambalo kwa kiasi kikubwa linaanzia katika ngazi ya familia.

Amesisitiza umuhimu wa kina mama kuwa mstari wa mbele kuchukua hatua za mapema za kuzuia udhalilishaji pia, amewasihi wanawake hao kujenga mazingira salama na kuhakikisha watoto wanapata malezi bora. 

Kwa upande wa wanadiaspora wamemuhakikishia Mama Mariam kuwa wataendelea kushirikiana naye katika jitihada zake za kuwahudumia wanawake, vijana na watoto

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.