Habari za Punde

Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan awaandalia Hafla ya Kuwapongeza Wachezaji wa timu ya Yanga, Ikulu Jijini Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Medali kama ishara ya shukrani kutoka kwa Rais wa Klabu ya Yanga Eng. Hersi Said wakati wa hafla ya kuipongeza timu ya Yanga iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 05 June, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Wachezaji na Makocha wa timu ya Yanga wakati wa hafla ya kuwapongeza kwa kufanikiwa kufika na kucheza mchezo wa Fainali ya Mashindano ya Shirikisho Afrika (CAF) nchini Algeria. Hafla hiyo ya kuwapongeza Yanga imefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 05 June, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi, wachezaji wa timu ya Yanga pamoja na wadau mbalimbali wa michezo wakati wa hafla aliyowaandalia kuwapongeza Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Wachezaji na Makocha wa Timu ya Yanga wakiwa kwenye hafla ya kupongezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Ikulu Jijini Dar es Salaam 


Viongozi, wachezaji wa zamani, waandishi wa Habari, watu maarufu, wasanii pamoja na wadau mbalimbali wa michezo wakiwa kwenye hafla ya kuipongeza timu ya Yanga iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es SalaamNo comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.