Habari za Punde

Wizara ya Utamaduni,Sanaa na Michezo Wametukumbudha Mbali Sana :Mhe. ZUNGU

 
Na Eleuteri Mangi, WUSM, Dodoma

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mussa Azan Zungu amewapongeza Uongozi wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kuweka bidhaa ambazo ndizo wanazifanyia kazi na kusema imewakumbusha mbali sana.

Naibu Spika Mhe. Zungu amesema hayo Juni 05, 2023 jijini Dodoma wakati akifungua maonesho ya Wizara hiyo na taasisi zake kabla ya kusomwa Bajeti ya mwaka 2023/2024 Bungeni jijini humo.

“Kwa kweli wametukumbusha mbali sana na vitu ambavyo nimeviona, wabunge wengi ambao nao wameviona, watu wengi tulikuwa tumeshavisahau, lakini kutokana na kuviona leo ni muhimu wote tukawa na utaratibu wa kivipitia vitu mbalimbali vya utamaduni wa taifa letu,

Tumeona namna nchi yetu ilivyopata uhuru, wapiganiaji wa huuru, rekodi na kumbukumbu zilizowekwa za wapigania uhuru wote wa taifa letu, tumeona speech ya Mwl. Nyerere ya mwaka 1962 Bungeni, ambayo sidhani kama kuna watanzania wengi wameisoma” amesema Naibu Spika Mhe. Zungu.

Ameongeza kuwa Mwl. Nyerere alitumia maneno mazuri ambayo alibainisha kuwa “Ingawa nasema niliapa, kiukweli tuliapa wote”, kila mwananchi amekula kiapo kulingana na maneno ya Mwl. Nyerere.

Kwa upande wake Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Balozi Dkt. Pindi Chana amesema wataendelea kushirikiana na Bunge katika masuala yote ya kuboresha kazi za sekta ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ili kuwaletea maendeleo watanzania.

Kama ishara ya ushirikiano mzuri kati ya wizara na Bange, Balozi Dkt. Pindi Chana amesema Wizara hiyo itawapatia wabunge vifaa vya michezo ikiwemo mipira pamoja na Kamusi Kuu ta Kiswahili toleo la 3 ikiwa ni vitendedea kazi kwa Wabunge wakati wa kutekeleza majukumu yao.

Katika ufunguzi huo Naibu Spika aliambatana na Waziri mwenye dhamana Balozi Dkt. Pindi Chana, Naibu Waziri Hamis Mwinjuma, Katibu Mkuu Saidi Yakubu, wakurugenzi, wakuu wa taasisi pamoja na watumishi wa Wizara hiyo.





No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.