Katibu Mkuu wa CCM, Komredi Daniel Chongolo akilakiwa na viongozi baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kigoma tayari kwa mkutano wa hadhara wa kuielimisha jamii kuhusu usahihi wa uwekezaji wa Bandari ya Dar es Salaam.
Tayari elimu hiyo imeshatolewa na CCM katika Kanda za Nyanda za Juu Kusini, Kanda ya Kusini, Kanda ya Kaskazini, Kanda ya Kati na Leo ni Kanda ya Magharibi.
Chongolo alipowasili mjini Kigoma amepokelewa na mabango yenye ujumbe mbalimbali wa kuunga mkono uwekezaji wa Bandari ya Dar es Salaam.
Akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Thobias Andengenye
Akivishwa skafu na vijana wa CCM baada ya kuwasili Ofisi za CCM Mkoa wa Kigoma.
Hamasa zilitawala wakati wa mapokezi hayo
Chongolo akisalimiana na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Kigoma, Josephine Genzabuke,
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
No comments:
Post a Comment