MAKAMU wa kwanza wa rais wa Zanzibar
(KUSHOTO) akiwa katika kikao kazi na watendaji wakuu wa ofisi yake leo tarehe
31.07.23. kushoto ni ni Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo Dk Omar Dad Shajak . Picha na Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais.
MAKAMU wa kwanza wa Rais wa Zanzibar (katikati shati nyeupe) akiwa katika kikao kazi na watendaji wakuu wa ofisi yake leo tarehe 31.07.23. kulia ni waziri wan chi ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais Mhe, Hasrous Said Suleiman na kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dk Omar Dad Shajak na kushoto kwa katibu ni Mkurugenzi wa Mipango sera na Utafiti Nd. Daima Mohammed Mkalimoto.
Picha na Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais.
Makamu wa
Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, amewataka watendaji mbali
mbali katika taasisi na Idara za serikali nchini kuzingatia na kufuata vilivyo sera za Idara zao kwakuwa ndio zenye miongozo
muhimu katika kufanikisha utekelezaji wa
malengo waliyopangiwa.
Mhe. Othman
ameyasema hayo alipokutana na watendaji wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Ofisi
yake katika kikao kazi cha kujadili utekelezaji wa malengo na mipango mbali mbali waliyojiwekea ndani ya wizara hiyo sambamba na kufahamu
changamoto walizonazo na kutafuta njia bora ya
pamoja kuzitatua.
Mhe. Othman
amesema kwamba sera zinapofuatwa na kusimamiwa vyema zinaweza kurahisisha utekelezaji wa mipango iliyopo na ijayo kwa mambo mbali mbali mbali na hivyo kuongeza
ufanisi na mafanikio kazini.
Amewataka
watendaji hao kuzidisha mashirikiano na watendaji mbali mbali wanaowasimami na
kwamba kuhakikisha wanawapongeza pale wanapofanya vyema katika utekekezaji wa
majukumu yao lakini na kuwaelekeza pale wanapoonekana kutotimiza wajibu wao
ipasavyo.
Amefahamisha
kwamba zipo baadhi ya taasisi serikalini
wanapopanga na kutekeleza mipango mbali mbali hawazingatii sera za taasisi
zao jambo ambalo ni nikinyume na
utungwaji wa sera hizo ambapo zinapofatwa hurahisisha mambo mengi ya
kiutendaji.
Aidha, Mhe.
Othman amewataka watendaji hauo kusimaia na kufuata kwa makini taratibu na
sheria za fedha kwa kuwa jambo hilo linapotokea huwa linaharibu taswira ya
ofisi na kiongozi anayesimamia taasisi hiyo.
Akizingunzia
suala la mapambano dhidi ya dawa za kulevya, Mhe. Othman amesema kwamba suala
hilo bado ni gumu kiutekelezaji na kwamba ni muhimu kwa jamii na viongozi
kubadilika na kulichukulia suala hilo kwamba ni la kitaifa badala ya kuliona
kwamba ni la mamlaka inayohusika na mapambano dhidi ya dawa za kulevya poekee.
Naye Waziri
wa Nchi Ofisi wa Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe. Harous Said Suleiman amesema
kwamba kuna umuhimu wa kuwepo mkakati wa kutolewa elimu kwa umma kwa masuala
mbali mbali yanayotekelezwa na taasisi na idara mbali ,mbali ili jamii iweze
kufahamu mambo yanayotekelezwa na serikali.
Kwa upande
wake Kamshina Mkuu wa Mamlaka ya
kupambana na kudhibiti dawa za Kulevya Kanal Burhan Nassor amesema
kwamba Mapambano dhidi ya dawa za kulevya Bado ni changamoto kubwa kulingana na
ukubwa wa tatizo lilivyo kwa kuwa bado madawa ya kulevya yanaendelea kuingia
Zanzibar kupitia njia mbali mbali.
Hata hivyo
amesema kwamba suala hilo pia linaendelea kuwa gumu kutokana na kukosa
mashirikiano kutoka kwa baadhi ya watendaji
katika taasisi mbali mbali za ulinzi na usalama jambo ambalo
linadhoofisha juhudi za mapambano hayo.
Aidha
amesema kwamba kutokana na hali hiyo ufanisi
katika mapambanoya Dawa za kulevya Zanzibar unaendelea kuwa changamoto na kuwa na mafanikio madogo
na kwamba kesi nyingi zimekuwa zikikosa ushahidi mahakamani na watuhgumiwa
kuachiwa huru .
Amesema
Mamlaka hiyo imefungua jumla ya kesi 449 Unguja na Pemba ambapo zipo katika hatua mbali mbali za
kisheria ambapo kati ya hizo 70 zipo katika hatua ya upelelezi, kesi 19 zipo
kwa mkemia Mkuu na 13 zipo kwa Mkurugenzi wa Mashitaka wakati kesi 36
zimefungwa na kesi 311.
Amesema
katika ya kesi 311 zilizofikishwa mahakamani kesi 187 zinaendelea, kesi 107
zimeachiwa huru na kesi 19 tu ndio
washitakiwa wametiwa hatiani kutokana na changamogto ya kukosa ushiorikiano
kutokahata kwa baadhi ya mahakimu na mashahidi huru ambao baadhi hupatiwa
vitisho kutoka kwa watuhumiwa.
Amesema
kwamba mamlaka hiyo inakusudia kuifanyia marekebisho sheria ya mamlaka hiyo ili
kutoia uwezo zaidi wa kuendeleza mapamnbao hayo
na kuondosha tatizo la madawa ya kulevya hapa Zanzibar .
Mwisho
Kitengo cha
Habari
Ofisi ya
Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar
31, Julai 2023.
No comments:
Post a Comment