Habari za Punde

Waziri Haroun ateta na watendaji wake

Katibu wa Tume ya kurekebisha Sheria Mussa Kombo Bakari akiwasilisha taarifa ya utendaji kazi wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi (OR) ,Katiba ,Sheria Utumisha na Utawala Bora Haroun Ali Sleiman kuangalia utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020-2025 ndani ya  Taasisi zilizopo chini ya Wizara yake.
Watendaji wa Tume ya kurekebisha Sheria wakiwa katika mkutano wa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji kwa Waziri wa Nchi (OR) ,Katiba ,Sheria Utumisha na Utawala Bora Haroun Ali Sleiman ikiwa ni muendelezo wa Ziara yake kuangalia utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi mwaka 2020-2025 ndani ya   Taasisi zilizopo chini ya Wizara yake.
Mwenyekiti wa Tume ya kurekebisha Sheria Khadija Shamata Mzee akizumza wakati akaimkaribisha Waziri wa Nchi (OR) ,Katiba ,Sheria Utumisha na Utawala Bora Haroun Ali Sleiman kuzungumza na watendaji wa Ofisi hiyo mara baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji katika Ziara yake kuangalia utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi mwaka 2020-2025 ndani ya  Taasisi zilizopo chini ya Wizara yake.
Waziri wa Nchi (OR) ,Katiba ,Sheria Utumisha na Utawala Bora Haroun Ali Sleiman akizungumza na watendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria katika muendelezo wa ziara yake kuangalia utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ndani ya Taasisi zilizopo chini ya Wizara yake.
 

Na Faki Mjaka -AGC


Taasisi za Serikali nchini zimetakiwa kuacha tabia ya kuingia katika hati za Makubaliano (MOU) na Mikataba mbali mbali bila kupata ushauri wa kisheria kutoka Afisi yaMwanasheria Mkuu Zanzibar.

Wito huo umetolewa na Waziri wa Nchi Afisi ya Rais katiba, sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Haroun Ali Suleiman alipofanya ziara katika Taasisi zilizo chini ya Wizara yake   kwa lengo la kusikiliza taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025.

Amesema ni makosa makubwa kwa Taasisi yoyote ya Serikali kuingia katika Mkataba wowote bila kuishirikisha Afisi hiyo kwa kudhani kuwa hakuna ulazima wa kufanya hivyo jambo ambalo ni hatari kwa maendeleo ya Taasisi husika na Serikali kwa ujumla.

Amesema zipo baadhi ya Taasisi hujiamini na kuingia Mikataba bila kuishirikisha Taasisi hiyo na linapotokea tatizo ndio ikiwemo la kushitakiwa ndio huanza kukimbilia kwa Afisi ya Mwanasheria Mkuu.
“Ukweli ni kwamba zipo baadhi ya taasisi hujiona wao wanajua zaidi, wakatayarisha mambo yao huko, wakikwama ndio wanaelekea kwa Mwanasheria Mkuu, hivi sivyo. Ni dhambi kubwa na hatari kwa Taasisi na Serikali kwa ujumla” alisisitiza Waziri Haroun.

Katika kuondoa changamoto hiyo Waziri Haroun ameiomba Afisi ya Mwanasheria Mkuu kuitisha Kikao cha Makatibu wakuu wote wa Wizara pamoja na Wakuu wa Taasisi ili kuwapa elimu kuhusu mwelekeo wa Serikali ya awamu ya nane katika kufunga mikataba mbali mbali.

Amesema inawezekana wapo baadhi ya Viongozi uelewa wao ni mdogo na matokeo yao hungia katika makosa bila kudhamiria kwa sababu tu ya kukosa ufahamu, hivyo watakapofahamishwa itawasaidia wao na serikali kwa ujumla.
Waziri Haroun alitolea mfano wa Mkurugenzi wa Serikali Mtandao aliyekuja ofisini kwake ambapo pamoja na mambo mengine alimtaka afike Afisi ya Mwanasheria Mkuu kuja kupata uelewa kuelekea dhamira ya taasisi hiyo kubadilika na kuwa Mamlaka ya Mtandao.

Waziri Haroun alitumia nafasi hiyo kuipongeza Afisi hiyo kwa mafanikio makubwa katika uendeshaji huku akiusisitiza uongozi kuwajengea uwezo Wafanyakazi wake katika nyanja mbali mbali za elimu.

“Awamu hii mambo ni mengi, naomba uongozi uongeze kasi ya kutoa fursa za masomo kwa wafanyakazi wote, mwenye diploma afanye shahada ya kwanza, mwenye shahada ya kwanza afanye ya pili na kuendelea ili Serikali iwe na watu mahiri wa kuitetea’’alinasihi Waziri Haroun.

Awali akiwasilisha Ripoti ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM yam waka 2020-2025 kwa kipindi cha 2020 hadi Julai 2023 Mwanasheria Mkuu Zanzibar dkt. Mwinyi Talib Haji alisema shughuli za usimamizi wa kesi, mikataba na uandishi wa sheria zimefanyika kwa ufanisi mkubwa.
Alisema katika kipindi hicho jumla ya kesi 139 zilisikilizwa mahkamani ambapo kesi 17 kati ya hizo zilifunguliwa katika kipindi hicho.

Aidha jumla ya kesi 15 zilimalizika na Serikali ilishinda jumla ya Kesi 13 na kushindwa katika kesi mbili.
Hata hivyo Dkt. Mwinyi amesema Afisi imechukua hatua na kukata Rufaa katika kesi hizoambazo ni “High Class Ltd Vs African Hotel & Tours Co. Ltd and AG” na “Yussuf Juma Yussuf Vs ZANTEL and AG”

Kwa upande wa Uandishi wa Sheria Mwanasheria Mkuu amesema, kwa kushirikiana naTaasisi husika, jumla ya Miswada 24 na Kanuni 101 zimeandaliwa, huku Matangazo mengine ya kisheria 446 yaliandaliwa na kutangazwa katika Gazeti Rasmi la Serikali.

Kuhusu usimamizi wa Mikataba amesema Sekta ya Mikataba imeimarika ambapo jumla ya Mikataba 2,087 imetolewa ushauri wa kitaalam, kati ya Mikataba hiyo 1,330 inahusu ununuzi wa bidhaa na huduma. Mikataba 371 inahusu ujenzi, 223 ni ushauri elekezi, 163 inahusu Kodi.

Akizungumzia changamoto za Afisi hiyo Mwanasheria Mkuu alisema inakabiliwa na ufinyu wa Jengo kutokana na ongezeko la Wafanyakazi huku usafiri hasa kwa wafanyakazi wa ofisi ya Pemba ukiwa ni changamoto.
katika ziara hiyo Waziri haroun alitembelea Ofisi za Tume ya kurekebisha Sheria , Skuli ya Sheria na Afisi ya Mwanasheria Mkuu Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.