Habari za Punde

Kudumaa kwa taaluma ya uandishi umerejesha nyuma maendeleo ya utamaduni wa kujua kusoma nchini
 Kukosekana taaluma ya uandishi wa vitabu nchini inachangia kurejesha nyuma maendeleo ya utamaduni wa kujua kusoma nchini

Ameyasema hayo Makamo Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Taifa (SUZA) Profesa Moh'd Makame Haji. Chuo cha SUZA kampasi ya Vuga Mjini Unguja.
Amesema,Takwimu zinaonesha ya kwamba ndani ya jamii bado wapo watu wasiojua kusoma na kuandika,na hii inatokana na taaluma ndogo ya uandishi wa vitabu na kusoma ili kuweza kuleta maendeleo ya kielimu nchini.
Aidha,amesema lengo la kuwepo kongamano hilo ni kuhamasisha jamii juu ya uandishi wa vitabu na kusoma ili kuleta maendeleo ya Elimu nchini.
Aidha, Profesa ametoa wito kwa jamii kufanya kazi ambazo zitasaidia jamii kupata uelewa, ujuzi ili kuweza kuleta maendeleo kwa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.
Hata hivyo,amewaasa waandishi wa vitabu kuwa na utamaduni wa kufanya tafiti zitakazosaidia kuandika vitabu sahihi vinavyokwenda na wakati.
Akiwasilisha mada ya kukosekana Kwa taaluma ya uandishi wa vitabu katika Elimu huchangia kurejesha nyuma utamaduni wa kusoma na kuandika.
Nae Mhadhiri Mstaafu wa Chuo Kikuu Cha Taifa (SUZA),Maalim Ali Mwalim Rashid ameeleza kuwa,tatizo la jamii kukosa maarifa ya uandishi wa vitabu husanabisha na mamlaka za Elimu nchini kutoingiza katika,somo la Uandishi wa vitabu katika ngazi ya Msingi na Sekondari.
Sambamba na hayo ameiomba Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kuingiza somo hilo ili jamii iwe na utamaduni wa. kusoma vitabu na kuweza kuandika.
Kwa upande wao washiriki katika kongamano hilo wameushukuru uongozi wa Chuo Cha SUZA kwa kuandaa kongamano hilo,na kuahidi kuyatumia vyema Mafunzo hayo ili lengo Hilo liweze kufikiwa.
Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano (WEMA ).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.