Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Mwinyi Awasili Nchini Cuba

Na.Mwandishi Wetu Havana,CUBA.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiambatana na Mama Mariam Mwinyi pamoja na ujumbe wake amewasili  Havana, Cuba kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali wa kundi la 77 na China.

Katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jose Marti Rais Dk. Alipokelewa na Balozi wa Tanzania nchini Cuba Mhe.Balozi  Humphrey Herson Polepole na maafisa wengine wa Ubalozi wa Tanzania na Cuba.

Ushiriki wake katika Mkutano huo ambao unatarajiwa kufunguliwa  tarehe 15 Septemba,Rais Dk.Hussein Ali Mwinyi anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan. 
Baadae  Rais Dk. Mwinyi atafungua rasmi Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Nchini Cuba.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.