Habari za Punde

Wizara ya Afya yaingia mkataba na Benjamin Mkapa Foundation WIZARA ya Afya Zanzibar imetiliana saini mkataba wa mashirikiano baina ya Benjamini Mkapa Foundation wa kuimarisha sekta ya afya hapa nchini.

Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar Dkt Amour Suleiman Mohamed amesema mkataba huo utaimarisha ushirikiano wa utaoji wa huduma za afya katika nyanja tofauti ikiwemo ya rasilimali watu.
Amesema Benjamini Mkapa Foundation imekuwa ikishirkiana na Serikali katika kuvitekeleza vipa umbele katika sekta ya afya ambavyo vimejumuishwa kwenye mkataba huo vya kuhakikisha wizara ya afya inafanya vizuri katika kufikia malengo ya utoaji wa huduma wa afya

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.