Habari za Punde

Mama Mariam Mwinyi Ametoa Rai Kuwekeza katika Elimu ya Mtoto wa Kike

Mke wa Rais wa Zanzibar , Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) Mhe.Mama Mariam Mwinyi ametoa rai kuwekeza katika elimu ya mtoto wa kike ili kumwezesha kiuchumi, kijamii husasan kujiamini kufanya maamuzi sahihi kuhusiana na afya ya uzazi na mpangilio kufikia  maendeleo endelevu kwa kuzingatia uzazi wa mpango na lishe bora kulingana na mahitaji ya idadi ya watu.

Mama Mariam Mwinyi ameyasema hayo leo tarehe 09 Oktoba 2023 akitoa salamu za nchi katika  ufunguzi wa Jukwaa la nne la Viongozi  Wanawake lililoandaliwa na Mke wa Rais wa Burundi Mhe. Angeline  Ndayishimiye lililofanyika ukumbi wa Hoteli ya Kiriri , Bujumbura Burundi.

Jukwaa hilo limefunguliwa rasmi na Waziri Mkuu wa Burundi Mhe.Gervais Ndirakubuca aliyemwakilisha Rais wa Burundi Mhe.Evariste Ndayishimiye. 

Wengine waliohudhuria ni Mke wa Rais wa Kenya Mhe.Mama Rachel Ruto, Mke wa Rais wa Rwanda Mhe.Mama Jeannette Kagame pamoja na wageni waalikwa  mbalimbali wakiwemo wawakilishi wa Mashirika ya Umoja wa Afrika , kikanda , wadau wa maendeleo na ujumbe kutoka China. 

🗓️09 Oktoba 2023

📍Bujumbura, Burundi

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.