Habari za Punde

Wananchi watakiwa kupima afya zao




 WANANCHI visiwani Zanzibar wametakiwa kujenga tabia ya kufanya uchunguzi wa afya zao ikiwemo macho ili kuweza kuondokana na athari mbali mbali ambazo zinaweza kujitokea athari katika macho.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Kinga na Elimu ya afya Zanzibar Dkt. Salim Slim huko Tumbatu katika maadhimisho siku ya uoni duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo terehe 12 ya mwezi wa kumi kila mwaka na ujumbe wa mwaka huu ni “penda macho yako ukiwa kazini”
Amesema iwapo wananchi watakuwa na tabia ya kufanya uchunguzi wa macho mara utasaidia kubaini mapema viashiria vinavyoweza kusababisha magonjwa sabambamba na kupatiwa matibabu stahiki na kwa wakati na kuepukana matatizo makubwa ikiwemo upofu.
Amewataka wananchi kufika katika vituo vya afya viliyo karibu nao kwa ajili ya hatua zaidi wanapohisi mabadiliko yoyote kwenye macho ikiwemo macho kuuma, kuwasha au kutokuona vizuri.
Dkt. Slim amebainisha kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kupitia Wizara ya Afya kwa kushirikiana na wadau wa Maendeleo inaendelea kusogeza huduma mbali mbali za afya ikiwemo za macho katika jamii ili kurahisisha upatikanaji wa huduma hizo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.