Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi tarehe 14/10/2023 ilijumuika na wananchi wanaoishi pembeni ya eneo tengefu la ufugaji wa pweza, Pongwe, kwa mavuno ya msimu wa Julai-Septemba, 2023.
Ufunguaji wa mavuno hayo ulishuhudiwa na Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Kati, Bi Marina Joel Thomas, Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi, Dr Aboud Suleiman Jumbe na Mkurugenzi wa Idara ya Uhifadhi wa Maeneo ya Bahari, Dr Makame O Makame.
Tanzania ni nchi ya kwanza inayozalisha pweza katika ukingo wa magharibi wa bahari ya hindi na kuwa kwa wastani nusu ya mavuno hayo yanatoka Zanzibar.
No comments:
Post a Comment