Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi amewasili Pemba jkwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili kuelekea shamrashamra za kutimiza miaka mitatu ya uongozi wake na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika Mikoa miwili ya Pemba.
Katika uwanja wa ndege wa Pemba amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mattar Zahor Masoud, na viongozi mbalimbali wa Serikali, vyombo vya ulinzi na usalama, Chama cha Mapinduzi na viongozi wa dini.
No comments:
Post a Comment