Habari za Punde

BENKI YA DUNIA YAENDELEA NA ZIARA KUANGALIA MIRAD IA IDA 20

Mkurugenzi Mkuu wa  Benki ya Dunia Axel Van Trotsenbung akipata maelezo kuhusiana na maendeleo ya mradi wa ufugaji wa samaki unaofadhiliwa na Benki hiyo huko Bumbwini Mafufuni Kaskazini A.


Na Sheha Sheha,    Maelezo 

Mkurugenzi Mwandamizi wa Benk ya Dunia Axel Van Tvotsenburg amesema Benki ya Dunia itaendelea kushirikiana na Tanzania katika uendendelezaji wa Miradi mbali mbali kwaajili ya kuleta maendeleo endelevu Nchini.

 

Akizungumza na wananchi wa mafufuni wilaya ya kaskazini "B" Unguja alipotembele miradi ya kimaendeleo katika Shehia hiyo amesema ameridhishwa na Maendeleo ya miradi hiyo hivyo Benki ya Dunia itaendelea kusaidia Miradi ya kimaendeleo ili kuwasaidia wananchi.

 

Naye Waziri wa Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Dk . Saada Mkuya Salum amesema Matunda yaliyopatikana katika uatekelezaji Miradi ya Benk ya Dunia Nchini yameijengea uaminifu Tanzania Jambo ambalo litahamasisha upatikanaji wa fedha zaidi kutoka Benk hiyo.

 

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Nchini Shadrack Nzirai amesema Taasisi yake inaendelea kuwawezesha wananchi Kupitia miradi mbali mbali ya uimarishaji wa uchumi wao ili kuondokana na umaskini.

 

Nao wananchi wa Mafufuni wameishikuru Benki ya Dunia kwa kuwasaidia katika Miradi ya kuwainua kiuchumi na kuahidi kuendeleza kuitunza miradi hiyo.

 

Viongozi wa Benk ya Dunia wanaendelea na mkutano wa siku tatu wa IDA 20 unaofanyika Visiwani Zanzibar.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.