Habari za Punde

CHAMA CHA MAPINDUZI CHA TOA SALAMU ZA POLE NA RAMBIRAMBI

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kina ungana na Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Dkt. samia Suluhu Hassan kutoa salaam za pole na rambirambi  kwa wananchi wa Wilaya ya Hanang mkoani Manyara kufuatia mafuriko yanayoendelea hadi sasa ambayo yamesababisha vifo vya watu na majeruhi Pamoja na uharibifu mkubwa wa Miundombinu mbalimbali, yakiwamo mashamba na makazi ya wananchi.

Kupitia taarifa hii, Chama Cha Mapinduzi kinawapa pole wote walioguswa na vifo hivyo kwa namna moja au nyingine, wakiwemo waliopoteza wapendwa wao, ndugu, jamaa, marafiki. Tunawatakia uponaji wa haraka majeruhi wote wa mafuriko hayo wanapoendelea kupata matibabu.

Chama Cha Mapinduzi kinatoa wito kwa wananchi waendelee kuchukua tahadhari na kuitaka serikali na vyombo vinavyohusika na uokoaji viendelee na jitahada ya uokoaji.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.