Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman akipokea maelezo kutoka kwa naibu Katibu wa Jumuiya ya Wafugaji nyuki Zanzibar Nd. Abdu Baruan (kulia) huko Kitogani wilaya ya kusini Unguja. Mhe. Makamu alifanya ziara kuona shughuli za ufugaji nyuki huko kitogani leo tarehe 13.12.2023. ( Picha na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.
Makamu
Kitogani na ZABA
13.12.20232
Mkoa wa
Kusini Unguja
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud
Othman, amesema kwamba ufugaji wa nyuki ni miongoni mwa mazao yenye fursa kubwa
kiuchumi kwa wananchi wanaojishughulisha na kazi hiyo jambo litakalochangia kukuza kipato chao na kuweza kupiga hatua
katika kupambana na umasikini.
Mhe. Othman ameyasema hayo huko Kitogani Mkoa wa Kusini
Unguja alipotembelea Jumuiya ya Wafugaji Nyuki Zanzibar ( ZABA), ili kuona
jitihada zinazofanywa na wanajumuiya hao katika kuendeleza kazi ya ufugaji
nyuki.
Mhe. Makamu amesema kwamba kutokana na hali hiyo kuna haja ya
suala hilo la ufugaji na uchakataji wa bidhaa za nyuki kulifanya kuwa ni jambo
la kitaifa kutengenezewa mazingira yatakayoleta faida zaidi kwa wananchi na taifa kwa jumla.
Hata hivyo, Mhe.
Makamu amesema kwamba suala la kuwepo sera na sheria makhusi ya mazao ya nyuki
na uchakataji wake ni changamoto ambayo serikali inahitaji kuifanyia kazi ili
kuliwekea mipango mizuri zaidi na kulifanya suala hilo la mazao ya nyuki kuliongezea tija
kwa wananchi na taifa kwa jumla.
Amesema kwamba kinachohitajika zaidi ni kujenga mazingira ya
kuweza kuzalisha asali na mazao mengine yanayotokana na asali ili kuweza kuuza
kwa bei kubwa kama zinavyofanya nchi nyengine mbali mbali duniani ambao
wamefaidika sana na suala hilo.
Amesema kwamba serikali inahitaji kujenga uwelewa zaidi kwa
wananchi na watendaji mbali mbali na kwa pamoja kulifanya zao hilo kwamba ni lakitaifa
ambalo linahitaji kuendelezwa kwa juhudi za pamoja hasa katika uchakataji wa
bidhaa za nyuki jambo litakalokuwa na manufaa makubwa na kueleta tija zaidi.
Ameongeza kwamba iwapo wafugaji wa nyuki wataweza kuzalisha
kwa wingi na kwa ubora kuliko ilivyo sasa pamoja na kujitangaza ipasavyo katika
masoko mbali mbali duniani zao hilo litaweza kuuzwa kwa thamani ya bei kubwa
kama ilivyo kwa nchi nyengine duniani
ambapo bei ya asali ni kubwa na yenye manufaa sana kwa wafugaji .
Amesema kwamba Zanzibar inabahati ya kuwa asili ya kuwa na
bidhaa zenye ubora sana na kwamba asali ya Zanzibar pia nimiongoni mwa zenye
ubora na inayoweza kuuzwa kwa thaman kubwa iwapo itachakatwa kiutaalamu na
kutangazwa zaidi katika masoko tafauti.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohammed Mahamoud,
amewahidi wanakikundi hao kwamba serikali ya mkoa huo itachangia gari nane za
fusi kwa jumiuya hiyo ili waweze kutengeneza eneo la maegesho ya magari kwa
wanaotembelea eneo hilo sambamba na kutoa pikipiki pamoja na kuchangia tangi la
maji ili kuwanga mkono umoja huo wa wafugaji nyuki.
Amesema kwamba mkoa huo una misitu mikubwa ya kitaifa miwili
na jumla ya misitu ya jamii ipatayo 25
ambayo iwapo itatumika vyema inaweza
kuwa ghala kubwa la asali kwenye mkoa huo.
Mapema naibu Katibu wa Umoja huo Abdu Baruan Abdalla ameomba
serikali kuwasaidia kutatua changamoto mbali mbaki za ushirika huo ikiwa ni
jitihada za kuboresha mazingira ya
ufugaji nyuki na uchakataji wa mazao yatokanayo na nyuki kuwa na faidia kwao na
taifa kwa jumla.
Mwisho.
Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar
Disemaba 13, 2023
No comments:
Post a Comment