Habari za Punde

Mchezaji wa Timu ya KVZ Akram Muhina Omar Ameweka Rikodi ya Kuwa Mchezaji wa Kwanza Kufunga Bao Katika Uwanja wa New Amaan Complex Zanzibar Baada ya Kufunguliwa

 

Mchezaji wa Timu ya KVZ Zanzibar Akram Muhina Omar akiwa katika mchezo wa Michuano ya Kombe la Mapinduzi Cup 2023/2024, na kuweka historia ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga bao katika Uwanja huo baada ya kufunguliwa kwa kukamilika kwake ujenzi wake mkubwa.

Ameandika bao lake la kwanza na la historia katika uwanja huo wa New Amaan Complex Zanzibar uliofunguliwa 27-12-2023 na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk.Hussein Ali Mwinyi, na katika ufunguzi huo kulikuwa na mchezo wa kirafiki kati ya Timu ya Taifa ya Zanzibar Heroes  na Timu ya Kilimanjaro Stars katika mchezo huo timu hizo zimetoka sare ya bila kufungana.

Akram ameandika bao lake la historia  katika michezo wa Kombe la Mapinduzi Cup 2023/2024 katika  mchezo uliofanyika 29-12-2023 kati ya Timu ya KVZ na Jamhuri , ameipatia Timu yake bao la kuongoza katika dakika ya 9 ya mchezo huo uliofanyika katika Uwanja wa New Amaan Complex Zanzibar 

Mshambuliaji wa KVZ Akram Muhina Omar (Halaand) jina lake litaekwa kwenye vitabu vya Historia ya Soka kuwa mchezaji wa kwanza kufunga bao kwenye Uwanja wa New Amaan Complex ambao umefanyiwa maboresho makubwa.

Bao hilo amelifunga katika dakika ya 9 ya mchezo kwenye Mashindano ya Kombe la Mapinduzi dhidi ya Jamhuri.

Ikumbukwe kwamba zaidi ya dakika 270 zimechezwa Uwanjani hapo pasipo kupatikana goli ukiwemo mchezo wa Zanzibar Heroes 0-0 Kilimanjaro Stars, Mlandege 0-0 Azam na Chipukizi 0-0 Vital'o.

Akram ataingia kwenye vitabu vya kumbukumbu kwa kufunga goli hilo na atazawadiwa Fedha Taslim Shilingi Milioni Moja (1,000,000).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.