Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi Ameweka Jiwe la Msingi Mradi wa Kituo cha Mabasi Kijangwani Wilaya ya Mjini Unguja.Ikiwa ni Shamrashamra za Miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiondoa pazia kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Kituo cha Mabasi Kijangwani Wilaya ya Mjini Unguja, na (kushoto) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar Mhe.Dkt.Saada Mkuya Salum,  ikiwa ni Shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,hafla hiyo iliyofanyika leo 31-12-2023 katika viwanja vya Mradi huo kijangwani
MUONEKANO wa moja ya majengo katika Mradi wa ujenzi wa Kituo cha Mabasi Kijangwani Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, lililowekewa Jiwe la Msingi la ujenzi wake leo 31-12-2023 na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, ikiwa ni shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Mhandishi wa Kampuni ya M+M Architects Co.Ltd Ismail Burhani Mvungi, akitowa maelezo ya michoro ya majengo ya Kituo cha Mabasi Kijangwani Wilaya ya Mjini Unguja, wakati wa hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la ujenzi huo leo 31-12-2023,ikiwa ni shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, na (kulia kwa Rais) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar Mhe.Dkt.Saada Mkuya Salum na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe.Idrisa Mustafa Kitwana na (kushoto kwa Rais) Mkurugenzi Mwendeshaji wa (ZSSF) Ndg. Nassor Shaban.
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) Ndg. Nassor Shaban akizungumza na kutowa maelezo ya Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Mabasi Kijangwani wakati wa hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ujenzi huo leo 31-12-2023, ikiwa ni shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar Mhe.Dkt.Saada Mkuya Salum akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmin Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi kuzungumza na Wananchi katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la Mradi wa ujenzi wa Kituo cha Mabasi Kijangwani Wilaya ya Mjini Unguja leo 31-12-2023.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia katika hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la ujenzi wa Mradi wa Kituo cha Mabasi Kijangwani Wilaya ya Mjini Unguja, ikiwa ni shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akifuatilia hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la ujenzi wa Mradi wa Kituo cha Mabasi Kijanwani Wilaya ya Mjini Unguja leo 31-12-2023 na (kushoto kwake) Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Mgeni Hassan Juma na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe.Idrisa Kitwana Mustafa
VIONGOZI mbalimbali wa Serikali wakifuatilia hutuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akihutubia katika hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Mradi wa ujenzi wa Kituo cha Mabasi Kijangwani Wilaya ya Mjini Unguja, ikiwa ni Shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
WAFANYAKAZI wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) wakifuatilia hutuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akihutubia katika hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Mradi wa ujenzi wa Kituo cha Mabasi Kijangwani Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, ikiwa ni Shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.