Habari za Punde

KINANA ASHIRIKI MKUTANO MKUU WA JIMBO LA RUANGWA

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana akiwa ameambatana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ambaye pia ni Mbunge wa Ruangwa, Kassim Majaliwa na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Lindi, Hassan Jarifu, wakiwa na viongozi, wanachama wa CCM na wananchi wakienda katika Uwanja wa Likangala mjini Ruangwa kuhudhuria Mkutano Mkuu wa CCM Wilaya ya Ruangwa.

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana, Waziri Mkuu ambaye pia ni Mbunge wa Ruangwa, Kassim Majaliwa wakiwa wamesimama baada ya kufika uwanja wa Likangala kuhudhuria mkutano  mkuu wa CCM Wilaya ya Ruangwa
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa kipindi cha miaka mitatu, katika Uwanja wa Likangala mjini Ruangwa
MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana akiwahutubia wana CCM na wananchi wa Wilaya Ruangwa alipokuwa mgeni rasmi katika Mkutano Mkuu wa CCM wa wilaya hiyo katika Uwanja wa Likangala mjini Ruangwa. Kupitia mkutano huo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliwasilisha taarifa ya utekelezaji wa ILANI ya Uchaguzi ya CCM kwa kipindi cha miaka mitatu. 
WAJUMBE wa Mkutano Mkuu wa CCM Wilaya ya Ruangwa wakicheza na kufurahia waliposhiriki mkutano mkuu wa CCM wa wilaya hiyo uliofanyika katika Uwanja wa Likangala mjini Ruangwa.
WAJUMBE wa Mkutano Mkuu wa CCM Wilaya ya Ruangwa wakicheza na kufurahia waliposhiriki mkutano mkuu wa CCM wa wilaya hiyo uliofanyika katika Uwanja wa Likangala mjini Ruangwa.
Mkurugenzi wa TOT, Khadija Omar Kopa Pamoja na Msanii wa Singeli Dotto wakitumbuiza katika Mkutano Mkuu wa CCM Wilaya ya Ruangwa uliofanyika katika Uwanja wa Likangala mjini Ruangwa 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.