Habari za Punde

Ziata katika Kaburi la Mwanamapinduzi Kanali Mstaafu Said Iddi Bavuai

Waziri wa  Utalii na Mambo ya Kale, Mhe Mudrik Ramadhani Soraga  akitoa wasifu wa Marehemu Kanal Mstaafu Said Iddi Bavuai  katika kaburi lake huko Shakani Wilaya ya Magharibi 'B' Unguja wakati wa kufanya ziara na kusoma dua.ikiwa  ni Maadhimisho  ya wiki ya Kuwaenzi Viongozi wa Kitaifa .na Waasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar.
Muongozaji dua Sheikh Sharif Abdulrahman wa Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar  akisoma dua ya Marehemu Kanal Mstaafu Said Iddi Bavuai katika kaburi lake Shakani Wilaya ya Magharibi 'B' Unguja wakati wa kufanya  ziara na kusoma dua,ikiwa ni Maadhimisho ya wiki ya Kuwaenzi Viongozi wa  Kitaifa na Waasisi wa Mapinduzi ya  Zanzibar .
Mmoja wa Mwanafamilia Rukia Saidi Iddi Bavuai akitoa shukrani Kwa niaba ya familia ya Said Bavuai huko Shakani Wilaya ya Magharibi 'B'katika Kaburi la Marehemu Kanal Mstaafu  Said Iddi Bavuai  wakati wa kufanya ziara na kusoma dua .ikiwa ni Maadhimisho ya wiki ya Kuwaenzi Viongozi wa Kitaifa na Waasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar
Picha na Khadija Khamis -Maelezo.

Na Khadija Khamis ,_Maelezo .01-04-2024

Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale, Mhe. Mudrik Ramadhani Soraga amesema Kanali Mstaafu Marehemu Saidi Iddi Bavuai alikuwa mstari wa mbele katika ukombozi wa Nchi  sio kwa kuhadithiwa bali alikuwa  mpambanaji katika kuupigania  Uhuru wa Zanzibar .

Akitoa kauli hiyo huko Shakani Wilaya ya Magharibi 'B'  Unguja  wakati wa kufanya ziara na kusoma dua katika kaburi la kanal Mstaafu Marehemu Saidi Iddi Bavuai .

Amesema Marehemu alikuwa nI kiongozi wa kupigiwa mfano Kwa namna ambavyo ameitumikia Nchi na Serikali yale.

Aidha amesema  Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar  Kwa kuthamini  juhudi za viongozi mbali mbali waliokwisha tangulia mbele ya haki imeamua kuandaa ratiba maalumu ya  kila mwaka kuyatembelea makaburi yao na kuwaombea dua pamoja na kupata fursa ya kukutana na wanafamilia.

Alifahamisha kuwa viongozi waliotangulia  walithaminiwa na Serikali za Awamu zote zilizopita na kuamini kwamba wataendelea kuthaminiwa na kuombewa dua Kwa kila mwaka .

Nae  Mmoja wa Wanafamilia  Rukia Saidi Iddi Bavuai akitoa shukrani Kwa niaba ya familia amesema ameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Kwa kuandaa  utaratibu huo wa kuonana na viongozi katika dua ya pamoja ya Mzee wao    

Amesema kushirikiana pamoja katika dua ya Mzee wao kunasaidia kujenga Imani na umoja katika familia na  Serikali Jambo ambalo litaimarisha  udugu na mshikamano.

Kwa Upande wa Muongozaji wa dua  Sheikh Sharif Abdulrahman  wa Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar akiongoza dua ya Marehemu  Kanal Mstaafu Saidi Iddi Bavuai na kumuomba Mwenyezi Mungu amughufirie madhambi yale na ampe Pepo ya daraja la  juu , Amin .
 
Ziara na dua za viongozi ni Maadhimisho ya wiki ya Kuwaenzi Viongozi wa Kitaifa, Waasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar na Katibu wa Kwanza wa chama cha Afro Shirazi pamoja na Siku ya Kumbukumbu ya Marehemu Sheikh Abeid Aman Karume

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.