Habari za Punde

Bandarini Taxi SACOS Wafanya Mkutano Mkuu 2024

Na Takdir Ali. Maelezo. 22.05.2024.

Mkurugenzi idara ya usalama kazini kutoka Wizara ya Nchi, Afsi ya Rais Uchumi na Uwekezaji Ali Mohd Nyanga amewataka Viongozi wa Sacos kushirikiana na wanachama wao ili kuweza kufikia malengo yaliokusudiwa ya kujikwamua na tatizo la umasikini.

 

Ameyasema hayo huko katika Ukumbi wa Studio Rahaleo wakati alipokuwa akifunguwa Mkutano Mkuu wa Bandarini Taxi Sacos mwaka 2024.

 

Amesema Sacos nyingi zinaanzishwa nchini, hazifikii malengo kutokana na kutokuwepo mashirikiano ya kutosha baina ya Viongozi na Wanachama.

 

Kwa upande wake katibu mtendaji wa chama kikuu cha ushirika cha kuweka na kukopa Zanzibar Zascu Abdallah Hassan Iddi amesema kazi kubwa wa chama hicho ni kutetea vyama vya akiba na mikopo, kutoa elimu, kutoa mafunzo, ushauri na kusimamia chaguzi zote za Sacos Zanzibar.

 

Aidha amevitaka vyama hivyo kufuata kanuni, taratibu na sheria zilizowekwa na Serikali kupitaia idara ya maendeleo ya vyama vya ushirika Zanzibar ili kuepuka migongano katika yake na Serikali.

 

“Vyama visiendeshwe kwa mazoea viendeshwae kwa mujibu wa katatibu, kanuni na sheria ili wanachama watu wapate imani na vyama vyetu ila pia na viongozi wetu jambo ambalo litaweza kuwasidia Wanaushirika huo.” Alisema Katibu huyo.

 

Nae Katibu Mkuu wa Bandari TAX Sacos Suleiman Ahmada Suleiman amesema lengo la mkutano mkuu wa mwaka 2023-2024 ni kuwafahamisha wanachama wao walichokifanya kwa kipindi cha mwaka mmoja ikiwemo makusanyo ya fedha, matumizi, miradi mbalimbali.


Amewataka wanachama kuweka hakiba kwa wingi ili kuweza kupata mikopo ya kuendesha Maisha yao sambamba na kulipa kwa wakati ili waweze kupata na wengine.

 

Amesema katika kuhakikisha wanauenuwa ushirika huo wameamua kuchukuwa gari mbili za mkopo ili ziweze kuwasaidia katika kuendesha harikari zao za kila siku.

 

Nao baadhi ya Wanachama wa wamewaomba viongozi wao kutumia vizuri nafasi walizopewa ili kuepukana na migogoro inayoweza kuleta mpasuko katika chama.

 

Aidha wamewaomba nidhamu wakati wanawahudumia wateja wao sambamba na kutoa stahiki za wanachama ikiwemo faida, na akiba na ubani wa ufiwa ili kuzidi kujenga mumoja, Upendo na Mshikamano miongoni mwao.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.