Habari za Punde

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan azungumza na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Gates Foundation Jijini Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Gates Foundation Bw. Mark Suzman yaliyofanyika kwa njia ya mtandao (Video Call) tarehe 10 Julai, 2024. Mazungumzo hayo yalilenga kuimarisha uhusiano baina ya Tanzania na Taasisi hiyo na kujadili maeneo mengine ya ushirikiano ikiwemo katika masuala ya afya, kilimo, uwezeshwaji wanawake kiuchumi, uchumi jumuishi, Elimu na matumizi ya  akili bandia (AI) katika maeneo tajwa. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.