RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Baraza la Maulamaa Zanzibar,baada ya kumaliza mazungumzo , walipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo na kujitambulisha leo 23-8-2024, mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Al hajj Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema kuna haja kwa Serikali
kuangalia kwa karibu miundombinu duni ya madrasa, maslahi ya walimu wa madrasa
na maimamu wa misikitini.
Al hajj Dk. Mwinyi, aliyasema hayo
Ikulu, Zanzibar kwenye mazungumzo na viongozi wakuu na wajumbe wa Baraza la Ulamaa
Zanzibar waliofika kumtembelea.
Amesema, miundombinu ya madrsara,
maslahi ya walimu madrsara na ma imamu wa misikitini nchini ni dhaifu mno, alisema
ni vyema Serikali kwa kushirikiana na vyombo vya kidini kuangalia njia nzuri ya
kufanyakazi na kusaidia namna ya kuzitatua changamoto hizo.
Akizungumzia suala la mmong’onyoko wa
maadili kwa jamii, Al haj Dk. Mwinyi alisifu juhudi za Baraza hilo kwa
kuendelea kutoa elimu kwa jamii licha ya tatizo hilo kuwa kubwa.
Pia, Alhaj Dk. Mwinyi ameupongeza
uongozi na wajumbe wa baraza hilo kwa jitihada zao za kutoa elimu ya ndoa kwa
wanandoa na warajis wa ndoa kwa Unguja na Pemba ili kupunguza matatizo na
migogoro ya ndoa kwenye jamii sambamba na kutoa fatwa kutokana na changamozo zinazo
ikabili jamii.
Kuhusu migogoro mbalimbali inayohusiana
na dini ya kiislamu kwenye jamii, Alhaj Dk. Mwinyi amelipongeza Baraza hilo kwa
weledi wa utatuzi mzuri wa migogoro hiyo, sambamba na kutatua hata viashiria
vinavyosababisha migogoro hiyo.
Vilevile, Alhaj Dk. Mwinyi hakuacha kulisihi
Baraza hilo kuendelea kuisimamia amani na utulivu kwa kutumia lugha moja
kupitia viongozi wao, maimamu misikitini pamoja na wanasiasa kwenye majukwaa
yao ili kuendeleza taifa lenye umoja na mshikamano.
Naye, Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh
Saleh Omar Kaab, alipongeza juhudi za maendeleo anazozisimamia Alhaj Dk. Mwinyi
hasa kwa kipindi kifupi cha uongozi wake, pia alimuahidi Al haj Dk. Mwinyi kumpa
ushirikiano wa hali ya juu kutoka kwa baraza hilo kupitia misingi ya quran,
hadithi, fikhi na tafsiri pamoja na kufuata miongozo na sunnah za Mtume (S.A.W)
hasa kwenye suala zima la kusimamia ustawi, amani na utulivu wa nchi.
Mapema, akizungumza kwenye kikao hicho,
Katibu Mtendaji kutoka Ofisi ya Mufti
Zanzibar, Sheikh Khalid Ali Mfaume amesema, miongoni mwa kazi za bara hilo
mbali na kumshauri na kumsaidia Mufti mkuu wa Zanzibar pia wanatoa elimu kwa
walimu wa madrasa, wanandoa na warajis wa ndoa kwa kuwakabidhi vibali baada ya
kuhitimu mafuzo, kutatua mambo mbalimbali ya dini ikiwemo kutoa fatwaa kwa
matatizo yanayoikabili jamii.
IDARA YA MAWASILIANO
IKULU, ZANZIBAR.
No comments:
Post a Comment