Habari za Punde

CCM yakoshwa na uamuzi wa Mzee Shamte

 


Na Leluu Majjid ,Zanzibar 

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesifu ujasiri na uzalendo alionao Mwanasiasa Mkongwe Baraka Mohamed  Shamte kwa kuweza  kukwepa ghiliba na hadaa za upinzani na kuendelea kuiunga mkono  CCM. 

Pia chama hicho kimesema uamuzi wake wa kuzungumzia maendeleo yaliopatikana kwa muda mfupi Zanzibar ameonyesha uungwana na kujua ukweli.

Msimamo huo umetolewa na Katibu  wa Kamati Maalum ya NEC Idara ya Itikadi na Uenezi, Khamis Mbetto Khamis,  aliyemtaja Mzee Shamte siku  zote amekuwa mtu jasiri.

Mbetto  alisema Mwasiasa huyo toka enzi za ASP baadae CCM,aliwahi kuteleza na kwenda kinyume na maadili ya Chama akavuliwa uanachama wake.

'Amethamini juhudu za  serikali ya awamu ya nane kwa hatua zinazochukuliwa na SMZ chini ya uongozi wa  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi. Taratibu za kumrudishia rasmi  uanachama wake zitaelekezwa"Alifafanua Mbetto  

Aidha alimtaja Mwanasiasa huyo ni mdau mkubwa wa maendeleo hivyo kutokana na kuvutiwa kwake na ufanisi wa SMZ,amejitokeza kuonyesha  hisia zake za kizalendo  .

"Ameitumikia Zanzibar tokea enzi za ukoloni .Amekuwa Naibu Katibu Mkuu ASP  Youth League .Ameshakuwa Katibu wa CCM Wilaya, Mwenezi  wa Wilaya ya Mjini Unguja Kichama. Alipovuliwa uanachama wake hakubabaika. Amekuwa muungwana taratibu zitaelekezwa kumrudishia uanachama wake" Alisema Mbetto. 

Aidha Katibu  huyo Mwenezi  alisema mzee huyo mara zote amekuwa akiitakia mema CCM,ndiyo maana hata alipofuatwa na baadhi ya vyama vya siasa  wakimtaka ajiunge navyo , aliwakatalia .

"Ameona utendaji wa Serikili ya Dk Mwinyi  inavyochapa kazi Amekubali ukweli kutokana na dhamira yake ya kujenga nchi na kutumikia wananchi na nchi"  Alieleza

Alisema CCM kwa kujua historia yake na mchango wake kwa Zanzibar,hivyo maelekezo ya vikao vya kikatiba vitafanyika ili kutimiza matakwa na kutoa  maazimio mengine.

"Awali hakutambua malengo na kusudio la Rais Dkt Mwinyi  katika mtazamo wa muda mfupi na mrefu .Kujikwaa si kuanguka .Ameelewa ,amejisahihisha na sasa atashirikishwa kusukuma mbele jahazi la maendeleo "Alisema Mbetto. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.