Habari za Punde

ZBC na ZIPA Wasaini Makubaliano ya Mashirikiano ya Kikazi

Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Ramadhan Bukini (kushoto) akitiliana saini na Mkurugenzi Mtendaji ZIPA Saleh Saad  Mohamed Mkataba wa Mashirikiano ya Kikazi  kati ya ZBC na ZIPA  kwa Mwaka Mmoja katika hafla ya Uzinduzi wa Kampeni ya Mkono  kwa Mkono Awamu ya Pili iliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Madinatul Bahr Mbweni Zanzibar. 
Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Ramadhan Bukini (Kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji ZIPA Saleh Saad  Mohamed wakionesha  Mkataba wa Mashirikiano ya Kikazi  kati ya ZBC na ZIPA  kwa Mwaka Mmoja  katika  hafla ya Uzinduzi wa Kampeni ya Mkono  kwa Mkono Awamu ya Pili iliofanyika Ukumbi  wa Hoteli ya Madinatul Bahr Mbweni Zanzibar.
Waziri wa Uchumi wa Bahari na Uvuvi Shaaban Ali Othman(Wapili kulia)akitoa hotuba ya Uzinduzi wa Kampeni ya Mkono kwa Mkono Awamu ya Pili hafla iliofanyika Ukumbi  wa Hoteli ya Madinatul Bahr Mbweni Zanzibar.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar Ndg. Salum Ramadhan Abdalla akitoa maelezo kuhusiana na Ushiriki wa Idara ya Habari Maelezo na Waandishi wa Habari   katika Uzinduzi wa kampeni ya Mkono kwa Mkono Awamu ya Pili ni kuwapa Habari wananchi mbalimbali kuhusiana na Miradi ya Maendeleo inayofanyika, hafla iliofanyika katika Ukumbi  wa Hoteli ya Madinatul Bahr Mbweni Zanzibar.

Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Ramadhan Bukini akisisitiza jambo wakati akimkaribisha Mgeni Rasmi katika  hafla ya Uzinduzi wa Kampeni ya Mkono  kwa Mkono Awamu ya Pili iliofanyika Ukumbi  wa Hoteli ya Madinatul Bahr Mbweni Zanzibar.
PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.16-10-2024



No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.