Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman akiondoa pazia na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Khamis Ramadhan Abdalla akiweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Mahkama ya Mkoa wa Kaskazini Pemba, ikiwa ni Maadhimisho ya Miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa
Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, amewataka watendaji wa mahakama Zanzibar
kuhakikisha kwamba wanatoa huduma bora kwa wanachi kwa kwenda sambamba na
uwekezaji mkubwa wafedha unaofanywa na serikali kwenye sekta hiyo hasa katika
suala la miundo mbinu na majengo ya kuleo.
Mhe. Othman ameyasema hayo huko
kinyasini wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba alipoweka jiwe la msingi wa
jengo jipya la kileo la Mahakama ya Mkoa wa kazikazi Pemba linalojengwa kwa gharama
ya Bajeti ya serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kama sehemu ya mkakati wa
serikali kuimarisha uduma za utoaji haki kupitia mahakama.
Amefaamisha kwamba ni vyema
watendaji wa Chombo hicho kikaimarisha huduma na upatikanaji wa haki kwa
wananchi ili maakama iiwe kimbilio lao badala ya kuikimbia kutokana na kukosa
Imani na chombo hicho muhimu .
Amesema kwamba mahakama pia zinapaswa
kuwa chombo cha kuchunguza matukio ya vifo vya ghafla na mengine ya namna hiyo
kwa kuunda tume zenye usimamamizi wa majaji wanaoaminika na jamii ili kuchunguza
matukio ya mauaji na ya vifo yanayojitokeza katika maeneo mbali mbali nchini
hivi sasa.
Amesema kwamba kufanya hivyo
kutajenga imani kubwa wa wananchi na chombo hicho pia kuweza kutimiza malengo
ya serikali ya kukimarishia miundombinu zikiwemo za majengo ya ofisi za majaji,
mahakimu, makadhi na watendaji weninge kwenye kada hiyo muhimu katika
upatikanaji wa haki.
Amesema kwamba jaji mkuu wa
Zanzibar anao uwezo na wajibu wa kisheria kusimamia uchunguzi wa kesi na matukio ya mauaji mbali mbali chini ya
utaratibu wa kuunda tume itakayosimamiwa na jaji ainayeaminika ndani ya jamii
Adha Mhe. Makamu amewaleza watendaji hao kwamba
hadhi ya chombo hico haitakuwepo kwa kuwa na majengo mazuri yaliyojengwa kwa
gharama kubwa pekee bali itatokana na namna mahakama katika ngazi mbali mbali
zinavyosimamia mashauri mbali mbali na haki ikaweza kupatikana na wananchi
kujenga Imani na chombo chao hicho.
Kwa Upande wake Jaji Mkuu wa
Zanzibar Khamis Ramadhan Abdalla amefahamisha kwamba hivi sasa mahakama mbali mbali zimeimairisha
na kuarakikisha kusikiliza mashauri mbali mbali na kuweza kumaliza kesi nyingi
kwa wakati na kwamba maakama nyingi zimefanikiwa
kumaliza mrundikano wa kesi kutokana na juhudi zinazofanywa kuimarishwa.
Amesema kwamba chombo ghicho pia
kimefanikiwa kupata mkopo wa dola milioni 30 ambazo zitatumika katika
uimarishaji wa makakama awamu inayofuata na kukifanya chombo hicho kuwa na
utendaji wa kileo ulioimarika kwa vifaa nba miundombinu ya kisasa lakini na
watendaji mahiri wenye utaalamu bora.
Naye Kaimu waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais Katiba na Sheria Shamata Shaame
Khamis amesema kwamba ujenzi wa majengo ya mahakama ni sehemu ya kuemdeleza
maboresho muhimu katika chombo hicho
kupitia bajeti inayotengwa na serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ili
kuwapatia wananchi huduma bora.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini
Pemba Salama Mbarouk Khatib amesema kwamba mkoa huo katika kipindi hiki cha
kuelekeea kilele cha kutimia miaka 61 ya mapinduzi jumla ya miradi 18
itazinduliwa na mingine kuwekewa mawe ya msingi na baadhi kufunguliwa.
Amewataka wananchi kuendelea
kushirikiana katika katika uendelezaji wa miradi ya maendeleo na kwamba kwa
upande wa mahakama hivi sasa inashuhudiwa kuwepo mabadiliko makubwa ya
kuboresha miundo mbinu ikiwemo ujenzi wa ofisi za kisasa.
Hafla hiyo ni mfululizo wa shughuli
mbali mbali zinazoendelea hivi sasa katika visiwa vya Unguja na Pemba ikiwa na
shamra shamra za kutimia miaka 61 ya mapinduzi matyukufu ya Zanzibar ya Januari
64 na kilele cha sherehe hizo kitafanyika Januari 12 mwaka huu wa 2025.
Mwisho
Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa
Kwanza wa Rais wa Zanzibar kupitia Kitengo chake cha Habari leo Ijumaa Disemba
27, 2024.
No comments:
Post a Comment