Habari za Punde

Mchezo Maalumu wa Mpira wa Miguu kwa Kati ya Viongozi wa SMZ na Viongozi wa Madhehebu ya Dini kwa Lengo la Kumuunga Mkono Rais Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi

Na.Khadija Mgeni. WHVUM

Waziri wa Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe.Tabia Maulidi Mwita  amesema Wizara ya Habari kushirikiana na Ofisi ya Rais wameunda mchezo maalumu wa mpira wa miguu kwa Viongozi wa SMZ na Viongozi wa madhehebu ya dini kwa lengo la kumuunga mkono Mhe.Dkt  Hussein Ali Mwinyi kwa maendeleo makubwa aliyoyafanya Nchini.

Ameyasema hayo katika Kiwanja cha Matumbaku, Wilaya ya Mjini , wakati wa uzinduzi na ugawaji wa Jezi kwa viongozi wa Timu ya SMZ ikiongozwa na Kocha, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo Fatma Hamad Rajabu ikiwa ni miongoni mwa Maadhimisho ya miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Amesema katika kuunga mkono kampeni ya Rais wa Zanzibar Mhe.Dk Hussein Ali Mwinyi timu ya viongozi wa SMZ wanatarajiwa kucheza fainali maalumu dhidi ya viongozi wa dini.

Aidha amefahamisha kwamba pambano hilo linatarajiwa kuchezwa kwa dakika 30 ,kabla ya mechi ya fainali ya Mapinduzi Cup mnamo Januari 13 ,2025  katika Kiwanja wa Gombani Pemba.

Amesema michezo inaleta umoja upendo na udungu sambamba na kuonyesha dini ya uislamu na madhehebu mengine haikatazi suala la michezo kutokana na kumjenga mtu kimwili na kiakili.

Meneja wa Timu ya Viongozi wa SMZ ,Mhe Tabia amesema Lengo la mchuano huo ni  kuonyesha umoja upendo na mshikamano kati ya viongozi wa dini na viongozi wa Serikali jambo ambalo litasaidia kuleta hamasa katika jamii.

‘’Mashndano hayo Tunakwenda kuwaonyesha Wananchi lazima tupendani tushirikiane kama Rais wa Zanzibar Mhe Hussein Mwinyi anavyohubiri umoja na upendo ndani ya nchi yetu ya Zanzibar “’amesema Mhe.Tabia.

Nae Kocha wa Timu ya  SMZ ,ambae pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo Fatma Hamad Rajabu Amesema Shekhe Nurdin kisk atakuwepo akiongozwa na viongozi wa dini wa madhehebu mbali mbali ili kuonyesha Viongozi hao pia wanapenda michezo.

Amewashukuru  Viongozi wa Wizara mbali mbali za Serikali pamoja na Viongozi wa Madhehebu ya Dini ikiwemo wa Mashekhe na Mapadri kwa Kuonyesha mashirikiano yao  kwa kujumuika pamoja katika kumuunga mkono Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk .Hussein Ali Mwinyi.

Kwa upande wa Wanamichezo hao wamesema timu yao imejipanga vyema  katika pambano hilo na kutarajia kuwafunga goli 3 - 0  wapinzani wao.

Mashindano hayo yametayarishwa na Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo kwa kushirikiana na Kurugenzi Ikulu .

Imetolewa na Kitengo cha Habari, Mawasiliano na Uhusiano

WHVUM

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.