Habari za Punde

Taasisi ya Inayojishughulisha na Utawala Bora Yafika Zanzibar

Na Rahma Khamis Maelezo  Zanzibar.

Waziri wa Nchi Ofisi  ya Rais Katiba, Sheria Utumishi na Utawala Bora Zanzibar Mhe Haroun Ali Suleiman amewataka wananchi kuendelea kudumisha  Amani na utulivu uliopo ili Nchi izidi kuwa salama na kuleta maendeleo.

 Wito huo ameutoa huko Ofisini kwake Mazizini mara baada ya kupokea Ugeni wa Taasisi inayoshughulikia masuala ya Utawala Bora (APRM )kutoka Namibia na Congo uliyofika kujifunza na kuangalia namna suala la Utawala Bora linavyokwenda Nchini.

 Amesema lengo la ujio hio ni kubadilishana  uzoefu na kuweka mikakati Bora ya kukuza dhana ya Utawala Bora ili  kuleta maendeleo.

Aidha amefahamisha kuwa kuongezeka kwa huduma muhimu za wananchi ikiwemo Afya na Elimu na kuwepo kwa uwazi kupitia Sema na Rais ni miongoni mwa  sehemu ya kuwepo kwa Utawala Bora.

Ameongeza kuwa Serikali ya awamu ya nane chini ya uongozi wa Dkt Mwinyi imeimarisha Serikali ya Umoja wa Kitaifa ambayo inahimiza suala la Utawala Bora nchini 

"Zanzibar baada ya Mapinduzi imeanzishwa mfumo wa vyama vingi ili kuwapa fursa wengine kuweza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi  hayo yote ni sehemu ya Utawala Bora nchini" alisema Waziri..

Hata hivyo ameeleza kuwa ujio huo utapata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali ya Zanzibar kwa ajili ya  kujifunza zaidi na kuitangaza Zanzibar.

 Katibu Mtendaji wa Taasisi hiyo (APRM) Tanzania  Lamau Mpolo  amesema kuwa wamefurahishwa kuona dhana ya Utawala Bora inatumika vizuri ndani ya Zanzibar .

Aidha amesifu Amani na utulivu uliyopo Zanzibar na kuitaka kuendelea kuitunza na kudumisha ili ibaki uendelee kubaki Nnchini

Aidha amefahamisha ipo haja kwao ya kujifunza zaidi kuwa suala hilo ili Taasisi hiyo iweze kuwa na nguvu pamoja na kuwashirikisha wananchi kutoa maoni yao.

Katibu huyo ameziomba Nchi hizo kudumisha ushirikiano uliyopo Kati yao ili uendelee kudumu kwa maslahi ya Taifa na wananchi wake.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.