MUONEKANO wa Jengo la Taaluma na Utawala la
Taasisi ya Sayansi za Bahari la Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, lililowekwa Jiwe
la Msingi la ujenzi wake na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi leo 5-1-2025,linalojengwa katika eneo la
Buyu Wilaya ya Magharibi “B” Unguja,ikiwa ni Shamrashamra za Maadhimisho ya
Miaka 61 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakisalimiana na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete,
alipowasili katika viwanja vya Chuo Buyu kwa ajili ya uwekaji wa Jiwe la Msingi
la Ujenzi wa jengo la Taaluma na Utawala la Taasisi ya Sayansi za Bahari Buyu
Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo 5-1-2025, ikiwa ni Shamrashamra za
Maadhimisho ya Miaka 61 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwnyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Prof.Bernadeta Killian akitowa
maelezo ya kitaalamu ya ujenzi wa jengo la Taaluma na Utawala la Taasisi ya
Sayansi za Bahari la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, linalojengwa katika eneo la
Chuo Buyu Wilaya ya Magharibi “B” Unguja na (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Rais
Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri
wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Tanzania Mhe.Prof. Adolf Mkenda na Katibu wa
Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said na (kulia
kwa Rais) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiondoa pazia na Mkuu wa Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Jakaya
Mrisho Kikwete, kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa jengo la Taaluma na Utawala
la Taasisi ya Sayansi za Bahari la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, linalojengwa
Buyu Wilaya ya Magharibi “B” Unguja, ikiwa ni shamrashamra za Maadhimisho ya
Miaka 61 ya Mapinduzi Matukufu wa Zanzibar
No comments:
Post a Comment