Habari za Punde

TANZANIA NA MISRI KUENDELEZA USHIRIKIANO KWENYE MIRADI YA UMEME -KAPINGA

Naibu Waziri wa Nishati, Mhe Judith  Kapinga ( wan ne kushoto) akiwa katika kwenye mradi wa umeme wa  Julius Nyerere (JNHPP) pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje, Uhamiaji na Wamisri waishio nje ya Jamhuri ya
Misri, Dkt Badir Abdelatty ( wan ne kulia)  tarehe 20 Machi 2025. Watatu kulia ni  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki Mhe Dannis Londo

Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Judith Kapinga, amesema Tanzania na Misri zitaendeleza ushirikiano  kwenye utekelezaji wa miradi ya umeme na kudunisha ushirikiano uliowekwa na waasisi wa nchi hizo.

Mhe Kapinga ameyasema hayo leo tarehe 20 Machi,2025, mkoani Pwani wakati alipofanya ziara katika mradi wa umeme wa  Julius Nyerere (JNHPP) pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje, Uhamiaji na Wamisri waishio nje ya Jamhuri ya Misri, Dkt Badir Abdelatty  ikiwa ni sehemu ya ziara ya  kikazi ya Waziri Badir na ujumbe wake.

‘’Tunamshukuru sana Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwani amekuwa msingi imara wa utekelezaji wa miradi huu wa  umeme na tumeona matunda halisi ya usimamizi wake.’’ Amsema Mhe.Kapinga

Amesema nchi ya Misri imetekeleza mradi huo wa JNHPP  kwa kuzingatia matakwa ya nchi ya Tanzania ambapo mpaka sasa mashine nane kati ya tisa zimewashwa na kuingizwa kwenye gridi ya Taifa

Akizungumza mara baada ya kutembelea na kujionea maendeleo ya mradi wa JNHPP, Waziri, Dkt Badir Abdelatty, amesifu ushirikiano wa muda mrefu uliopo kati ya Tanzania na Misri na kuishukuru Tanzania kwa  kuiamini nchi yake kutekeleza mradi huo wa JNHPP, kwani utawanufaisha wananchi wa Tanzania walio wengi hususani wale wanaozungukwa na eneo la mradi.

Amesema nchi za Afrika zinapaswa kujivunia uwepo wa miradi ya umeme kwa maendeleo ya waafrika wenyewe na kuahidi kuwa Misri itaendeleza ushirikiano na Tanzania kwenye utekelezaji wa miradi mingine kama hiyo

Kwa upande wake  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki Mhe Dannis Londo amesema, Tanzania na Misri zitaendeleza ushirikiano wa kidiplomasia ulionao ili kufungua fursa mbalimbali za kiuchumi hususani kwenye miradi ya sekta ya Nishati

Ziara hiyo.imehudhuriwa na  Balozi wa Tanzania nchini Misri, Balozi wa Misri nchini Tanzania, Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Mafuta,  Dk.James Mataragio, na viongozi mbalimbali kutoka Wizara ya Nishati naWizara  ya  Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.



Cap

Naibu Waziri wa Nishati, Mhe Judith  Kapinga ( wan ne kushoto) akiwa
katika kwenye mradi wa umeme wa  Julius Nyerere (JNHPP) pamoja na
Waziri wa Mambo ya Nje, Uhamiaji na Wamisri waishio nje ya Jamhuri ya
Misri, Dkt Badir Abdelatty ( wan ne kulia)  tarehe 20 Machi 2025. Wa
tatu kulia ni  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje anayeshughulikia masuala
ya Afrika Mashariki Mhe Dannis Londo

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.