Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitazama bidhaa mbalimbali alipotembelea banda la Maonesho la Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) kabla ya kufungua Kongamano la Chama cha Kisima cha Mafanikio kwenye Viwanja vya Olasiti Garden jijini Arusha, Aprili 13, 2025. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Kisima cha Mafanikio, Esther Kimweri , wa pili kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania ( BASATA) , Dkt. Kedmon Mapana na kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Sanaa za Maonyesho kutoka Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) Lilian Shayo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama bidhaa mbalimbali alipotembelea banda la maonesho la Masai Market Arusha lililo chini ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kabla ya kufungua Kongamano la Chama cha Kisima cha Mafanikio lililofanyika kwenye viwanja vya Olasiti Garden jijini Arusha, Aprili 13, 2025. Kushoto ni Flament Kivuyo na wa pili kushoto ni Sarah Robert wote kutoka Masai Market Arusha
Wazri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Zaituni Iddi (kulia) ambaye ni mwanachuo wa fani ya Umeme wa Majumbani kutoka VETA Arusha, alipotembelea banda la maonesho la VETA kabla ya kufungua Kongamano la Chama cha Kisima cha Mafanikio kwenye viwanja vya Olasiti Garden jijini Arusha, Aprili 13, 2025. Wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Kisima cha Mafanikio, Esther Kimweri.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na viongozi wengine wakiimba Wimbo wa Taifa wakati Waziri Mkuu alipofungua Kongamano la Chama cha Kisima cha Mafanikio kwenye viwanja vya Olasiti Garden jijini Arusha, Aprili 13, 2025. Kulia kwake ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Paramagamba Kabudi na kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Chama cha Kisima cha Mafanikio, Esther Kimweri
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza alipofungua Kongamano la Chama cha Kisima cha Mafanikio kwenye viwanja vya Olasiti Garden jijini Arusha.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua nembo ya Chama cha Kisima cha Mafanikio baada ya kufungua Kongamano la chama hicho kwenye viwanja vya Olasiti Garden jijini Arusha, Aprili 13, 2025. Kushoto ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Paramagamba Kabudi na kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Kisima cha Mafanikio, Esther Kimweri.
Baadhi ya washiriki wa ufunguzi wa Kongamano la Chama cha Kisima cha Mafanikio wakimsikiliza mgeni rasmi Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipozungumza kwenye viwanja vya Olasiti Garden jijini Arusha, Aprili 13, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
No comments:
Post a Comment