Na Sabiha Khamis Maelezo 06.05.2025.
Ofisi ya Msajilli wa Hazina Zanzibar limeanzisha Jukwaa la kwanza la Wakuu wa Taasisi za Umma linalotarajiwa kuwa ni sehemu ya kujenga mshikamano kwa viongozi hao pamoja na kuimarisha utendaji unaolenga kuleta mafanikio ya kiuchumi na kijamii Zanzibar.
Akitoa taarifa kwa Waandishi wa Habari Msajili wa Hazina Zanzibar Waheed Ibrahim Mohamed Sanya huko Golden Tulip amesema Jukwaa hilo limetoakana na maono ya Ofisi hiyo pamoja na utekelezaji wa agizo la Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla katika Jukwaa la Wakuu wa Taasisi za Umma Tanzania Bara lililofanyika Zanzibar Januari, 2025.
Amesema kuwa wakuu wa taasisi za umma wana majukumu ya uwekezaji kwa umma katika kuendeleza ubora wa huduma, uvumbuzi wa kuongoza na kuchochea ukuaji endelevu wa kiuchumi.
“Mazingira ya kisasa ya kiuchumi na kiutendaji yanaendelea kwa kasi katika kufikia ubora wa shirika kunahitaji uongozi wenye maono na ushirikiano”, alisema Sanya.
Ameeleza kuwa Jukwaa hilo la kihistoria limelenga kuwakutanisha wakuu wa taasisi za umma na binafsi kutoka sekta mbalimbali ili kubadilishana mawazo, kujadili changamoto zinazofanana katika utekelezaji wa majukumu, kubadilishana uzoefu wa kiuongozi na kuanzisha mikakati ya pamoja ya kuboresha ufanisi na uwajibikaji katika taasisi hizo.
Msajili Sanya amefahamisha kuwa Jukwaa hilo litatumika kuwa ni msingi wa ushirikiano wa kimkakati, kukuza mazungumzo kwa kiwango kikubwa, kubadilishana maarifa, kutatua changamoto zilizopo, kufungua fursa na mitandao kati ya viongozi.
Nae Mwenyekiti wa Jukwaa la Wakuu wa Taasisi za Umma Zanzibar (Zanzibar CEOs Forum) Juma Burhan Mohamed amesema lengo kuu la Jukwaa hilo ni kufikisha huduma kwa wananchi, kutatua changamoto ambazo zinazikumba taasisi za umma pamoja na kutengeneza fursa kwa taasisi binafsi na wananchi kuweza kujua na kukutana na wakuu wa taasisi za umma.
Amesema kupitia Jukwaa hilo wataweza kuwaweka pamoja
wakuu wa taasisi za umma ili kuwarahisishia wananchi
kutatua changamoto zao na kujua fursa zinazopatikana kwa
upande wa Serikali na sekta binafsi na kuzifahamu fursa hizo
ambazo zitaweza kusaidia kwa lengo la kukuza uchumi wa
Zanzibar.
Kwa upande wake CEO wa Taasisi ya Wakurugenzi Tanzania
Dkt. Said B. Kambi amesema kuwa Taasisi hiyo ipo tayari
kushirikiana na Ofisi ya Msajili wa Hazina Zanzibar ili
kusaidia kuwajengea uwezo viongozi wa taasisi za umma na
binafsi.
Jukwaa hilo la kwanza la Wakuu wa Taasisi za Umma
litafanyika kwa muda siku 3 kuanzia 11 hadi 13, 2025 mgemi
rasmi katikaJukwaa hilo anatarajiwa kuwa Makamu wa Pili
wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, kauli
mbiu ni “Uongozi bunifu na Mashirikiano ni Muhimu ili
kufikia Maendeleo Endelevu Zanzibar”.
Msajili wa Hazina Zanzibar Waheed Muhammad Ibrahim Sanya akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Jukwaa la Taasisi za Umma wenye lengo la kuleta Umoja ,Mshikamano na Ushirikiano,ambao unatarajiwa Kuanza Tarehe 11,12,13,hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar.
No comments:
Post a Comment