Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametunukiwa Medali ya Mother of the Nation Order kutoka kwa
Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu Mtukufu Sheikh Mohamed bin Zayed Al Nahyan.
Medali hiyo iliwasilishwa kwake na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje
wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Mhe. Sheikh Abdullah Bin Zayed Al Nahyan
Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 05 Mei, 2025.
Aidha, Medali hiyo ni moja kati ya Medali za juu kabisa kutoka kwa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE). Medali hiyo hutolewa kutambua mchango Kiongozi katika kuleta maendeleo endelevu kwa jamii yake. Serikali ya UAE imetambua mchango mkubwa wa Rais Dkt. Samia katika kuwaletea Watanzania maendeleo endelevu ambayo yanaendana na Sera za UAE za maendeleo endelevu katika kijamii, uwezeshaji wanawake na ushirikiano wa kimataifa.
Sheikh Abdullah aliwasilisha salamu
kutoka kwa Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu Mtukufu Sheikh Mohamed bin Zayed
Al Nahyan na kuwatakia kheri wananchi wa Tanzania katika maendeleo pamoja na
ustawi zaidi. Pia alisisitiza kuimarishwa zaidi uhusiano wa kudumu baina ya
nchi hizo mbili na kusisitiza umuhimu wa kupanua ushirikiano katika sekta
muhimu.
No comments:
Post a Comment