Na. Takdir Ali.
Mwakilishi wa Jimbo la Bumbwini Mhe. Mtumwa Peya Yussuf amewataka Vijana kukiamini na kukichaguwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kiendelee kushika Dola na kuleta Maendeleo kwa Wananchi wake.
Ameyasema hayo hivi karibuni, mara baada ya kukabidhi vifaa vya Skuli kwa Wanafunzi waliopata Division One na Michipuo pamoja na kukabidhi Mashine za kusukumia Maji katika Jimbo la Bumbwini Wilaya Kaskazini B Unguja.
Amesema lengo la kukabidhi vifaa hivyo ni kuwawezesha Wanafunzi kusoma kwa bidii ili waweze kuwa Viongozi wazuri wa hapo baadae.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo hilo, Mhe. Mbarouk Juma Khatib amesema Chama Cha Mapinduzi kipo mstari wa mbele katika kutekeleza Ilani kwa vitendo hivyo amewataka kuendelea kukipa ushindi kwa maslahi yao na Taifa kwa ujumla.
Aidha amewasisitiza Wanafunzi kuacha mambo ya anasa na badala yake wajikite zaidi katika masomo yao sambamba na kuheshimu Wazazi na Waalimu wao.
Nao Wanafunzi waliokabidhiwa zawadi hizo, wameahidi kusoma kwa bidii pamoja na kuvitunza vifaa hivyo ili viweze kuwasaidia katika masomo yao.
Hafla ya kukabidhi Vifaa vya Skuli kwa Wanafunzi wa Jimbo la Bumbwini, waliopata Divition One na waliopasi Michipuo, wamekabidhiwa vitu mbalimbali ikiwemo, Photocopy Mashine, Computer, Laptop na Mashine za kusukumia Maji ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Ofisi ya Zanzibar Tunu Juma Kondo.
By Takdir Ali.
No comments:
Post a Comment